The House of Favourite Newspapers

Nay, Shilole Kuipeleka Wapo Dar Live

0

NA MWANDISHI WETU: GAZETI LA IJUMAA WIKIENDA

STAA wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ anatarajiwa kuungana na msanii mwenzake, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ katika bonge la shoo lijulinakalo kama Usiku wa Wapo, Mei 20, mwaka huu ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala- Zakhem jijini Dar.

Akizungumza na Over Ze Weekend, Nay alisema kuwa, baada ya kusikia kilio cha mashabiki wengi wa muziki wake wakimtaka kuipeleka Wapo Dar Live sasa yupo tayari kukata kiu yao.

“Watu wangu wa Mbagala,Temeke, Tandika na Dar es Salaam kwa ujumla kilio chenu nimekisikia na Wapo kwa mara ya kwanza itashushwa ndani ya kiwanja chako cha Dar Live nikiwa na mwanangu Shilole.

“Listi kamili bado inakujia hivyo ni wakati wako kutega sikio na kusoma Magazeti ya Global kujua zaidi,” alisema Nay.

Mbali na shoo hiyo, Mei 13 kunatarajiwa tena kuwa na shoo ya nguvu katika kiwanja hicho kutoka kwa kundi kongwe la Muziki wa Taarab, Jahaz Modern.

Leave A Reply