The House of Favourite Newspapers

Nay wa Mitego anasa kwa mrembo wa Marekani

0

nayMkali wa ngoma ya Hip Hop, Nyumbani Kwetu, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.

MAHABA niue! Mkali wa ngoma ya Hip Hop, Nyumbani Kwetu, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amenasa kwa mtoto matata wa Kitanzania aishiye nchini Marekani ajulikanaye kwa jina la Stella Tillya ‘Chagga Baby’.

Ubuyu kutoka katika chanzo chetu unasema kwamba, kwa kipindi kirefu wawili hao wamekuwa katika uhusiano wa kimapenzi lakini hawakuweka wazi mpaka pale penzi liliponoga na kuanza kuandikiana posti za kimalovee katika mitandao ya kijamii hususan Instagram.

stella tillyaMtoto matata wa Kitanzania aishiye nchini Marekani ajulikanaye kwa jina la Stella Tillya ‘Chagga Baby’.

“Kumbe mlikuwa hamjazinyaka? Mbona sasa hivi ndiyo habari ya mjini! Shamsa tupa kule. Walianza kimyakimya mpaka penzi lilipowanogea na kuanza kuliweka wazi,” kilisema chanzo kilicho karibu na Nay.

Chanzo hicho kilikwenda mbali zaidi na kusema kwamba sasa hivi Nay haoni wala hasikii kwa mrembo huyo ndiyo maana anajiweka wazi mpaka kwenye Mtandao wa Instagram.

Mara baada ya kupenyezewa ubuyu huo, gazeti hili kupitia kachero wa kitengo cha OFM aliingia mzigoni na kufanikiwa kubamba mawasiliano ya kimalovee kati ya Nay na Chagga Baby.

Mara baada ya kuweka kibindoni ushahidi wa SMS kupitia kwa mtu wa karibu na Nay aliyeziiba katika simu yake, gazeti hili likamvutia waya Nay ili atoe ufafanuzi wa penzi hilo kwani hana muda mrefu tangu wamwagane na mwigizaji wa Kibongo, Shamsa Ford.

“Kaka usiwe na presha, hivi vitu vya ndani kabisa, vikiwa poa, kila kitu kitakuwa wazi,” alisema Nay.

Ikumbukwe kwamba kabla ya Nay kuzama katika penzi la Chagga Baby, aliwahi kutoka ‘kimalovee’ na mrembo aliyezaa naye, Siwema kabla ya kuangukia katika mikono ya muigizaji Shamsha ambaye naye alimbwaga.

Leave A Reply