Nay Wa Mitego Baada Ya Kuachiwa Na Jeshi La Polisi Afunguka – Video
Baada ya taarifa kusambaa zikimhusisha Msanii wa BongFleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kufunguliwa madai ya Uchochezi, Wakili wake, Jebra Kambole ambaye amethibitisha kuwa Nay wa Mitego kuitikia wito wa Jeshi la Polisi Kituo cha Kati-Dar kwa tuhuma za uchochezi kupitia baadhi ya mashairi ya wimbo wake wa ‘Amkeni’
Jebra amesema mteja wake ametoa maelezo na kukanusha tuhuma hizo akieleza kuwa nia ya Mashairi yake ni kuonesha upungufu kwenye Utawala kwa nia ya kurekebisha. Nay wa Mitego amepewa dhamana baada ya kutimiza masharti na ameambiwa kama kutakuwa na hatua za kisheria atajulishwa
Kuhusu Madai ya Nay wa Mitego kuzuiwa na BASATA kufanya matamasha, amesema hakuna taarifa rasmi kutoka BASATA, japokuwa BASATA walikuwa wakiwasiliana na Maafisa Utamaduni wa Mikoa ambao ndio walimnyima Mteja wake vibali. Amesema BASATA imempa Nay wa Mitego wito wa kwenda Ofisini kwao bila Mwanasheria Septemba 8, 2023