The House of Favourite Newspapers

Nay wa Mitego, Rich Mavoko Kulikoni?

0

WAKALI wa muziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki anayetamba kwa ngoma yake ya WAPO na Rich Mavoko kutoka Lebo ya Wasafi (WCB) inayomilikiwa na Diamond Platinumz wamejikuta wakijibizana mitandaoni baada ya Mavoko kutupia picha na maneno yaliashiria ujio wa ngoma yake mpya wakati akisikilizia hali ya kisiasa hapa nchini kwa sasa.

Mavoko ameandika kupitia Instagram;

Haya Mkimaliza Mambo Zenu Za Siasa Mtupe Tarehe Na Sisi Tufumue Hiii 📺 #Showme

Saa 18 baadaye, Nay wa Mitego naye akachukua picha ile ile aliyotupia Mavoko, aka-repost na kuandika huku akitamba kuwa ngoma pekee inayoweza kutusua kwa sasa ni ngoma yake ya WAPO.

Alichokiandika Nay kupitia Instagram;

Haya Mkimaliza Mambo Zenu Za Siasa Mtupe Tarehe Na Sisi Tufumue Hiii 📺 #ShowmeNAOMBA MUENDELEE KUSUBILI, MAY BE MPAKA MWAKANI 2018, NDO MTAANZA KUJISHUGHULISHA NA MASWALA YA KUWAIMBIA WANA NCHI.

MWAMBIENI NA BABA YENU PIA AWE MPOLE KWASASA ALEE WATOTO. KAZI TULIYO NAYO IKIENDA SAWA TUTA WARUHUSU MUENDELEE KUBURUDISHA WANA NCHI. TUNATAKA MAMBO YAENDA SAWA KWANZA✊🏿.
Wimbo wetu wa TAIFA ni #Wapo LINK ON MY BIO☝🏾️

Leave A Reply