Chalinze, Pwani: September 21, 2020: Wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule ya Msingi ya Chalinze mkoani Pwani wamehimizwa kusoma kwa juhudi ilikutengeneza maisha yao ya baadaye huku wakipewa changamoto ya kujitahidi kilawakati kuwa bora katika masomo yao na kwa kila kitu wanachofanya.
Hamasa hiyo imetolewa mapemawiki na Meneja wa Benki ya Kitaifa ya Biashara (NBC) Tawi la Samora Bi ZubeiderHaroun wakati akikabidhi mifuko 75 ya saruji kwa shule hiyo ikiwa ni hatua yabenki kuboresha miundombinu shuleni hapo hususani kwa kujenga choo chawanafunzi wenye mahitaji maalum.
Bi Zubeider aliwasihiwanafunzi hao kuwa elimu inaweza kuwapeleka mbali na kutimiza ndoto zao, kwa hivyowanahitaji kusoma kwa juhudi katika masomo yao huku akiwasisitiza kutokatatamaa hasa wanapopata changamoto katika safari zao za masomo.
“Kwa hivyo nawasihi muwekejuhudi katika masomo yenu ili kwa ajili ya faida ya maisha yenu ya baadae kwa kuwa elimu ni ufunguo ambaounafungua milango ya maisha yote. ” alisisitiza
Aliongeza kuwa benki hiyoitaendelea kusaidia maendeleo ya Elimu na ikiwemo kwa wale walio na mahitajimaalum ili kuboresha mfumo wa elimu jumuishi nchini.
“Kama benki tumejitolea kabisa kusaidia ujenziwa hitaji hili muhimu la miundombinu ya katika shule hii ili kuboreshaupatikanaji wa elimu hususani kwa wanafunzi wenye uhitaji maalum.’’ Alisema.
Pia, Bi Zubeider alitoa witokwa taasisi zingine na watu binafsi kuchangia kwa shule na vituo vya elimu kamanguzo muhimu kuelekea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Akipokea msaada huo BiAufemia Ngweta, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo aliishukuru Benki ya NBCkwa msaada huo na utashi wake katika kusaidia ukuaji wa elimu katika Wilayahiyo. Pia alitoa wito kwa wadau zaidi kusaidia shule hiyo.
“Hapa shuleni kunawatoto wenye ulemavu tofauti, kuna wale walio na ugonjwa wa kupooza kwa ubongoambao wanahitaji vifaa vingi vya kuchangamsha akili zao ili waweze kujifunzavitu mbalimbali kama ufundi na ujuzi mwingine kwa maendeleo yao ya baadaye. Kwahivyo juhudi zaidi zinahitajika kuhakikisha tunawafundisha vyema. ”Bi Ngwetaalifadhaika
Alimshukuru pia Bi Zubeidakwa kuwahamasisha wanafunzi hao, akibainisha kuwa ni matumaini yake wanafunzihao watabadilisha mawazo yao nakuthamini kwamba watu wenye mahitaji maalum wanaweza kuishi na kufaulu maishanihususani kupitia elimu.
Wanafunzi wa Shule ya Msingiya Chalinze walishukuru Benki hiyo kwa msaada huo huku wakiaahidi kufanyavizuri kitaaluma sambamba na kutoa wito kwa jamii iendelee kuwasaidia iliwaweze kutimiza ndoto zao.