The House of Favourite Newspapers

NBC Yaahidi Kuwekeza Katika Mifumo ya Kibenki ya Kidijitali ili Kuongeza Tajriba kwa Wateja

0

BENKI ya NBC imeahidi kuwekeza zaidi katika huduma za kibenki za kidijitali ili kuongeza urahisi wa upatikanaji wa huduma kwa wateja pamoja na tajriba yao.

Akizungumza na wateja wa Benki hiyo tawi la Mlimani City wakati wa uzinduzi wa mwezi wa huduma kwa wateja, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, alisema Benki hiyo inaendelea kupanua ‘mtandao wake kikawaida na kidijitali ili kukidhi matakwa ya wateja.


“Tutaendelea kuwekeza zaidi katika mifumo ya kibenki ya kidijitali na kupanua mtandao wetu wa huduma ili kuboresha urahisi wa upatikanaji wa huduma kwa wateja wetu na uzoefu wao wakati wakibenki nasi.

“Katika mwaka huu, tumefungua matawi mawili mapya moja likiwa Bungeni Dodoma na Kigamboni Dar es Salaam, lakini pia tumewekeza kwa kiasi kikubwa katika bidhaa zetu za kibenki kwa njia ya simu za NBC Kiganjani na NBC-Connect ambayo ni jukwaa la kimtandao maalum kwa makampuni” alisema.

Katika jitihada za kuimarisha ushirikiano na uhusiano wake na wateja wake, Benki ya NBC, inayojulikana kwa ustadi wa ubunifu, inaungana na dunia nzima kusherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja ya kila mwaka, kwa mwaka huu ikiwa na kauli mbiu “Sherehekea Huduma.”

Katika wiki hii, Benki ya NBC inatarajia kutumia kauli mbiu “Tunakuthamini” kuwaonyesha na kuwatambua wateja wake kwa kuifanya Benki ya NBC kuwa benki chaguo lao la kwanza

“Ahadi yetu kwa wateja wetu ni kwamba tutaendelea na jitihada zetu za kuimarisha utoaji wa huduma za benki kwa kutoa huduma bora na kuwa karibu kila wakati na wateja wetu kulingana na kauli mbiu ya benki yetu isemayo ‘Urahisi Kila Mahali’ katika kuhakikisha kuwa tunawasikiliza wakati wote na pengine kupita matarajio yao” Sabi alibainisha.

Kwa mwaka 2022, benki imeendelea kuimarisha huduma zake kwa kufanya maboresho kadhaa katika utoaji wa huduma kwa wateja ikiwa ni pamoja na kupanua mtandao wa huduma za benki ili kuwasogeza karibu wateja wake. ambapo pamoja na matawi 47 kote nchini, hivi karibuni benki hiyo ilifungua matawi mapya katika mikoa ya Dodoma na Dar es Salaam.

Benki hiyo pia imefanya maboresho makubwa ya huduma za ATM, ambazo kwa sasa zimefikia mashine 183 na kuongeza mtandao wa Mawakala wa NBC hadi mawakala zaidi ya 7000 kote nchini.”Tajriba na kuridhika kwa wateja wetu ni sehemu ya juu ya ajenda zetu.
Katika Benki ya NBC tunajivunia kuwa na wasiwasi na wateja wetu na kuridhika kwao ndilo lengo letu kuu. Tunaelewa urahisi wa huduma unaoletwa na ubunifu wa kidijitali na tuko tayari kutumia fursa hiyo katika eneo hilo la kibenki” alisisitiza.

Sabi pia aliwashukuru wateja wa benki hiyo kwa kuendelea kuiamini na kuiunga mkono Benki ya NBC na kuifanya kuwa benki ya kwanza chaguo lao.

“Zaidi ya yote napenda kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutuamini na kutufanya tuwe hivi tulivyo leo. Tunashukuru maoni yao ambayo yalitupa alama za juu katika utafiti wa benki wa Net Promoter Score (NPS) kwa wastani wa zaidi ya 50% katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo,” aliongeza.

Leave A Reply