The House of Favourite Newspapers

NBC Yapongeza Juhudi za Koplo Wa Jeshi la Polisi Kwa Kuhimiza Kuvaa Barakoa

0
Koplo Brown Twaibu Msoke akipokea zawadi ya fedha kutokana na kuielimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuvaa barakoa katika kupambana na gonjwa la corona.

Benki ya NBC leo imetambua juhudi mahususi za Jeshi la Polisi Tanzania na maofisa wake katika kipindi chote cha mlipuko wa homa kali inayosababishwa na virusi vya corona (Covid-19) . Katika matukio mbali mbali ya kipekee, maofisa kwa Jeshi la Polisi Tanzania wameonyesha hekima ya hali ya juu na dhamira ya kuwatumikia, kuwalinda na kuhakikisha Watanzania wanatekeleza maelekezo ya wataalam ya jinsi ya kupambana na ugonjwa wa corona.

Aidha, benki hiyo ikishirikiana na Jeshi la Polisi Tanzania pia imemtambua na kumpongeza Koplo Brown Twaibu Msoke kwa kuielimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuvaa barakoa katika kupambana na gonjwa la corona. Koplo Taibu alijizolea umaarufu baada ya video ikimuonyesha akiwahimiza abiria kwenye daladala kufuata maelekezo ya serikali kama kuvaa barakoa, kutosimamisha abiria kwenye usafiri wa umma na kukaa umbali wa mita moja siyo kwa kujilinda tu bali kuwalinda na
wengine.


Akiongea katika hafla hiyo, Mkuu wa Mawasiliano wa NBC, David Raymond Kigwile alisema “Kufikia maamuzi ya kumpongeza Koplo Taibu haikuwa kitu rahisi kwa benki yetu, hususan kwa sababu vitendo vyake vya kishujaa vinaendana na msimamo wa benki yetu katika kupambana na virusi vya Covid-19.

” Itambulike kuwa Benki ya NBC pia imechukua hatua madhubuti kupamba na kuenea kwa virusi hivyo kama kuwa benki ya kwanza kuweka vitakasa mikono katika ATM zake zote nchini, utekelezaji wa nafasi ya mita mbili katika matawi yake. Benki ya NBC pia itaendelea kuwahamasisha na kuwaelimisha wafanyakazi wake na Watanzania kwa ujumla jinsi ya kumpambana kwa ugonjwa huo.

Aidha Kamanda wa Polisi Ilala,  Zuberi Chembera alisema, “Koplo Twaibu ameonyesha mfano mzuri wa kuhamasisha jamii juu ya uvaaji wa barakoa kwa dhumuni la wananchi kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya maambukizi ya virusi vya korona. Kitendo hicho ni mfano wa kuiga na kinahitaji pongezi ya pekee hususan kipindi hiki ambacho dunia nzima inapambana na janga hili.

 

Pamoja Benki ya NBC kumtunuku Koplo Brown Msoke fedha taslim TSHs. 1,000,000 na kumfungulia akaunti katika benki hiyo, Jeshi la Polisi Tanzania pia limemzawadia Koplo Twaibu kiasi cha TSHs 200,000 na cheti maalumu kutoka kwa Kamanda wa Polizi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.

 

Katika kuendeleza dhamira ya kuelimisha jamii matumizi sahihi ya barakoa, Benki ya NBC imezindua kampeni yake mpya ya #NBCBarakoaChallenge. Pamoja kuhimiza uvaaji wa barakoa, kampeni ya #NBCBarakoaChallenge itakayoendeshwa kupitia mitandao ya kijamii ya NBC inaangalia pia kuwakumbusha na kuelimisha Watananzania juu ya umuhimu wa kuzingatia tabia
kinga ili kuzuia Covid-19.

Jinsi ya kushiriki Barakoa Challenge
● Jipige picha ukiwa umevaa barakoa.

● Post kwenye ukurasa wako wa Instagram ukiwa na hashtag #NBCMaskChallenge.
● Watag watu watatu uwaandikie ujumbe wa kuwakumbusha kuvaa barakoa.
Post yenye likes nyingi zaidi kujishindia simu janja aina ya Samsung A10s kila wiki.
Hakikisha akaunti yako haiko private ili tuweze kuona post yako.

Vigezo namsharti kuzingatiwa Kuhusu.

Leave A Reply