AKRIBANI nchi 33 zinatarajia kushiriki mkutano 13 wa Taasisi za Jumuiya ya Skauti wakike bara la Afrika (Taasisi ya Girl Guide) nchini Tanzania na kuwakutanisha wajumbe kutoka nchi hizo ambao ni wanachama wa World Association of Girl Guides and Girl Scous (WAGGGS).
Nchi hizo zinakutana kwa lengo la kutathmini hatua walizopiga kwa miaka mitatu iliyopita,tathmini ya Changamoto na mafunzo yaliyotokana na janga la Uviko 19,Kuweka mikakati mipya na kuchagua Uongozi wa kipindi kingine cha miaka mitatu kuanzia sasa.
Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaam na Kamishna Mkuu wa Jumuiya ya Skauti wakike Tanzania,Wakili Mary Richard alisema mkutano huo kufanyika nchini ni nafasi ya kuona na kujifunza kutoka kwa nchi zingine namna ambavyo wanaendesha shughuli zao za guiding.
Alisema mkutano huo pia utakuwa ni sehemu ya kukuza ufanisi na utendaji wa Chama kwani utaleta kundi la watu zaidi ya 120 nchini.
“Katika Mkutano huub,kutakuwa na hafla za ufunguzi kufunga na usiku wa Utamaduni ambapo inatarajiwa kufanyika Agosti 22 hadi 26,mwaka huu katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre,”
alisema na kuongeza