The House of Favourite Newspapers

Ndaruke Kuiongoza CCM Kibiti Miaka Mitano Ijayo

0
Mshindi wa pili kwenye uchanguzi wa ndani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibiti kwenye nafasi ya Mwenyekiti Abdujabiri Malombwa (kushoto) akimpongeza mshindi wa uchanguzi huo Juma Kassim Ndaruke baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi hio kwenye uchanguzi huo ambao ulifanyika jumapili 2 Oktoba 2022

 

 

Kwenye nafasi hiyo ambayo wagombea walikuwa watatu, Ndaruke alishinda kwa kupata kura 428 dhidi ya 385 za Malombwa huku mgombea wa tatu Abdallah Mpili akipata kura 7. Kuchanguliwa kwa Ndaruke kuna maanisha ya kuwa ndio atakuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibiti kwa miaka mitano ijayo (2022-2027).

Mbunge wa Jimbo la Kibiti Pwani, Twaha Mpembenwe akimpongeza Ndaruke.

 

 

Akizungumza na Wajumbe wa Mkutano wa chama hicho ngazi ya wilaya ambao ndio walikuwa na wajibu wa kupiga kura, Mwenyekiti huyo mpya wa wilaya ya Kibiti Juma Kassim Ndaruke alisema kuwa ni fahari kuona wajumbe wakuwapa nafasi za uongozi ndani ya chama ni hii inaonyesha ni kwa kiasi ngani CCM ilivyo wekeza kwenye kukuza vijana.

Wanachama wa CCM Wilaya ya Kibiti yenye kata 16 wakimshangilia Ndaruke baada ya kutangazwa mshindi.

 

 

‘Nachukua fursa hii kwanza kumshukuru Mungu, wajumbe pamoja na kila mmoja wetu aliyeshiriki kwenye uchanguzi. Naomba kusema kuwa hapa aliyeshinda sio Ndaruke mbali CCM ndio imeshinda’.

 

‘Tunapokwenda kuanza kazi na uongozi upya nataka kukuchukua fursa hii niwaambie kuwa tutaenda kujenga CCM imara yenye dira na ambayo itakuwa na uwezo wa kuisimamia serikali ili kuhakikisha ya kwamba miradi ya maendeleao kwenye wilaya yetu inatekelezwa pamoja na kumalizika kwa wakati’, alisema Ndaruke ambaye pia ni Mwenyekiti wa UVCCM mstaafu wa wilaya hiyo’.

 

Akizungumza baada ya kukubali matokeo, mpinzani wa karibu wa Ndaruke na ambaye pia alikuwa anatetea nafasi hiyo Malombwa alisema ‘Nachukua fursa hii kumshukuru Mwenyekiti wetu mpya na kusema kuwa nimekubali ya kuwa nimeshindwa kihalali kabisa. Lazima tukumbali kuwa uongozi ni kupokezana vijiti, muda wangu wa utumishi kama Mwenyekiti wa wilaya umemalizika na kwa sasa kijiti namuachia Ndugu Ndaruke’.

 

Kwenye uchaguzi huo, kulikuwepo na nafasi ya Mkutano Mkuu wa Mkoa ambao walioshinda ni Ashura Matimwa na Uwesu Mtandika na nafasi Mkutano Mkuu Taifa ambao walioshinda ni Ally Seif, Khalid Mtalazaki na Rehema Mkumba.

Leave A Reply