Ndayiragije Ataja Kilichompeleka Ufukweni

KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Etienne Ndayiragije, amesema kuwa sababu ya kuonekana katika fukwe za Escape One hivi karibuni, akifuatilia mazoezi ya baadhi ya nyota wa Stars ni ratiba yake binafsi ya mazoezi na halihusiani na yeye kusimamia mazoezi hayo.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Ndayiragije alisema alikuwepo ufukweni hapo kwa ajili ya kufanya mazoezi binafsi na kwa bahati nzuri akawakuta baadhi ya nyota wake wa Stars wakijifua, hivyo naye kujiunga kutazama mazoezi hayo.

 

“Ni kweli nilikuwepo katika fukwe za Escape One lakini haikumaanisha kuwa nilikuwa nasimamia au kuongoza mazoezi hayo, hapana.

 

“Nilienda pale kufanya mazoezi binafsi kama ilivyo kawaida yangu na kwa bahati nzuri nikawakuta vijana wakijifua, nikajiunga kuwaangalia,” alisema Ndayiragije.

 

Ndayiragije alikabidhiwa mikoba ya kuifundisha Stars baada ya kuiongoza klabu hiyo katika michezo sita, ameshinda mitatu, sare mbili na kupoteza mechi moja.

Stori: Joel Thomas, Dar es salaam

SHANGWE la MASHABIKI baada ya LIGI KUFUNGULIWA – “Yule RAIS Ana BUSARA SANA”


Loading...

Toa comment