The House of Favourite Newspapers

Ajali; Ndege Iliyobeba Wanasoka wa Brazil Yaanguka Colombia, Yaua 76, Watano Wanusurika 

mabaki

Mabaki ya ndege iliyoanguka.

ndege

ajali

Kabla ya kuanza safari timu hiyo ilipiga selfie hizi.

ndege

Ndege iliyoanguka hii hapa.

majeruhi

Mmoja wa wachezaji wa klabu ya Chapecoense, Alan Ruschel (27) akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kutolewa kwenye ndege hiyo.

majeruhi-2

Alan Ruschel akipelekwa hospitali kwa matibabu.

mabaki

Mabaki mengine ya ndege hiyo.

majeruhi-mwingine

Mmoja wa majeruhi aliyenusurika kwenye ajali hiyo akipatiwa huduma ya kwanza.

waliobaki-nyumbani

Wachezaji ambao hawakusafiri na timu hiyo wakiwa na simanzi katika vyumba vya kubadili nguo.

NDEGE iliyokuwa imebeba watu 81, wafanyakazi tisa na abiria 72 ikiwemo timu ya soka ya klabu ya Chapecoense ya Brazil imeanguka katika sehemu ya milima nchini Colombia wakati inakaribia Mji wa Medellin na kuua watu 76 huku watano pekee wakinusurika.

_92705602_colombiamedellin464

Ndege hiyo ya kukodisha iliyokuwa ikitokea Bolivia, ilikuwa na timu ya  soka ambayo ilikuwa icheze katika fainali ya Kombe la Amerika ya Kusini dhidi ya timu ya Atletico Nacional ya Medellin. Hivyo, fainali hiyo imeahirishwa.

Ripoti zinasema ndege hiyo yenye leseni namba CP 2933, ilianguka saa 4:15 jana usiku baada ya kupata hitilafu katika mfumo wake wa umeme na ilielezewa na Meya wa Medellin, Federico Gutierrez, kama “janga kubwa”,  huku akiongeza kwamba  inawezekana kuna watu walionusurika.

Imeelezwa kuwa baada ya ajali ndege hiyo ilivunjika katika vipande viwili na kupelekea vifo vya watu 76 huku watano pekee wakinusurika wakiwemo wachezaji watatu wa Chapecoense ambao ni beki Alan Ruschel, makipa Danilo Padilha na Jacson Follmann pamoja na abiria wengine wawili Rafael Correa Gobbato na Ximena Suarez.

Baadhi ya picha zilizowekwa mitandaoni zinawaonyesha wachezaji ambao hawakusafiri na timu hiyo wakiwa na simanzi katika vyumba vya kubadili nguo.

brazils-chapecoense-players-pose-for-pi

Kikosi cha timu hiyo.

halotel-strip-1-1

Comments are closed.