The House of Favourite Newspapers

Ndege Iliyombeba Makamu wa Rais wa Malawi Yaanguka

0
Abiria saba akiwemo Saulos Chilima na wahudumu watatu wa kijeshi walikuwa kwenye ndege hiyo ndogo ya jeshi la Malawi.

Wanajeshi, polisi na walinzi wa misitu wanaendelea kuitafuta ndege ya kijeshi iliyotoweka ikiwa na makamu wa Rais wa Malawi, mke wa rais wa zamani na watu wengine wanane.

Ndege iliyombeba Makamu wa Rais Saulos Chilima mwenye umri wa miaka 51 na mke wa rais wa zamani Bakili Muluzi, Shanil Dzimbiri ilitoweka Jumatatu asubuhi wakati ikiwa safarini kutoka mji mkuu wa taifa hilo la Kusini mwa Afrika, Lilongwe, kuelekea mji wa Mzuzu, katika upande wa kaskazini. Safari ambayo huchukua dakika 45.

Akilihutubia taifa moja kwa moja kwenye televisheni Rais Lazarus Chakwera alisema waongoza safari za ndege walimwambia rubani wa ndege hiyo kutojaribu kutua katika uwanja wa ndege wa Mzuzu kwa sababu ya hali mbaya ya hewa na kumtaka arudi Lilongwe.

Waongoza safari za ndege kisha wakapoteza mawasiliano na ndege hiyo na ikatoweka kwenye mtambo wa rada. Chakwera aliapa kuwa shughuli za utafutaji zitaendelea hadi ndege hiyo itakapopatikana. “Najua hii ni hali ya kuvunja moyo. Najua sote tuna hofu. Nami pia nina wasiwasi. Lakini nataka kukuhakishieni kuwa nitatumia raslimali zote zilizopo kupata iliko ndege hiyo. Na nina matumaini kuwa tutawapata manusura.” Abiria saba na wahudumu watatu wa kijeshi walikuwa kwenye ndege hiyo ndogo inayomilikiwa na jeshi la Malawi.

Kamanda wa jeshi la Ulinzi la Malawi Paul Valentino Phiri amesema kuwa huenda ndege hiyo ilianguka katika Msitu wa Chikangwa lakini haijapatikana. Amesema operesheni za utafutaji na uokozi zinakwamishwa na ukubwa wa eneo la msitu na hali ya hewa yenye ukungu mwingi.

RAIS SAMIA ANAHUTUBIA BAADA ya KUPOKEA GAWIO – MICHANGO KUTOKA MASHIRIKA NA TAASISI ZA UMMA

Leave A Reply