The House of Favourite Newspapers

Ndege Ndefu Zaidi Duniani Yatayarishwa Kibiashara na Abiria (PICHA)

 

NDEGE ndefu zaidi duniani ipo tayari kwa ajili ya kuanza kutengenezwa kwa ajili ya kibiashara na abiria.

 

Hatua hiyo inakuja baada ya sampuli ya awali ya ndege hiyo, Airlander 10,  yenye thamani ya pauni milioni 32  (Sh. bilioni 94.9) – ambayo ni mjumuiko wa ndege na meli inayopaa – ‘kupumzishwa’ rasmi baada ya kufaulu majaribio ya mwisho.

 

Kutokana na mafanikio hayo, kampuni iliyobuni ndege hiyo ya Hybrid Air Vehicles (HAV) yenye maskani yake Bedford, Uingereza, imepewa ruhusa na mamlaka ya usafiri wa anga wa kiraia wa nchi hiyo, Civil Aviation Authority (CAA), kuanza uzalishaji wa aina hiyo ya ndege.

 

Awali Oktoba 2018, kampuni hiyo ilipewa kibali cha usanifu kutoka mamlaka ya usalama wa usafiri wa kiraia barani Ulaya European Aviation Safety Agency (Easa).

 

Airlander 10 baada ya kuanguka Novemba 18, 2017 wakati wa safari ya majaribio

 

Stephen McGlennan, ambaye ni mtendaji mkuu wa kampuni ya HAV amesema mwaka 2018 ulikuwa mzuri na kwamba kibali cha Easa kilikuwa ni ishara njema kubwa.

 

Amesema kwa sasa azma ya kampuni yake ni kutengeneza ndege aina ya Airlander 10 kwa ajili ya biashara na abiria.

 

 

“Sampuli ya awali imetimiza kazi yake kwa kutusaidia kupata takwimu na taarifa muhimu tulizokuwa tukizihitaji ili kuvuka kutoka hatua ya mwanzo ya majaribio mpaka utengenezwaji wa ndege halisi,” amesema.

 

Kwa sasa matarajio ni kwamba ndege ya kibiashara itakatiza mawingu ikiwa na abiria  mwanzoni mwa miaka ya 2020.

 

 

HAV ilitenga kitita cha pauni milioni 32 baada ya sampuli ya awali kudondoka, na kuwaarifu wanahisa wake kuwa hicho ndicho “kiwango cha juu zaidi cha bima”.

 

Vibali kutoka CAA na Easa sasa vinaipa kampuni hiyo “nafasi imara ya kuanza uzalishaji”.

 

HAV ilifanya majaribio ya awali ya Airlander 10 kutoka katika eneo lake la awali la uwanja wa ndege wa Cardington mwezi Agosti 2016 lakini walihama eneo hilo Juni mwaka jana.

 

 

Mwezi Julai wakatangaza mipango yao ya kutoa “huduma za kifahari” pale ambapo majaribio yote yatakapomalizika kwa mafanikio.

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO.

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.