The House of Favourite Newspapers

Ndege ya FlyDubai Yaanguka na Kuua 62

0

FlyDubai_737-800_A6-FDB

FlyDubai Boeing 737 -800

WATU 62 wamepoteza maisha dunia baada ya ndege ya FlyDubai Boeing 737 -800 kupata ajali wakati ikijaribu kutua katika uwanja wa ndege wa Rostov-on-Don nchini Urusi usiku wa kuamkia leo.

Crash-APNdege hiyo ilivyowaka moto.
Crash-AP1 Waliopoteza ndugu zao kwenye ajali hiyo wakiomboleza.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari hiyo, FlyDubai Boeing 737 -800 hufanya safari zake kati ya Dubai na Rostov-on-Don ilikuwa imetoka Dubai na kupewa flight namba FZ981, na kwamba hali ya hewa ilibadilika ghafla mita chache kabla ya kutua uwanjani hapo ndipo rubani akajaribu kutua umbali wa mita 100 kutoka uwanja wa Rostov-on-Don uliopo Jimbo la Rostov.

Crash-AP2-1Inasemekana kuwa, ndege hiyo ilizunguka kwa takribani saa mbili kabla ya kufanya jaribio la pili la kutua mita 100 kutoka uwanjani hapo kufuatia hali mbaya ya hewa eneo la uwanja. Taarifa zimeongeza kuwa baada ya kuanguka ndege hiyo ilivunjika na kushika moto papo hapo.

Crash-AP6Waliokufa kwenye ajali hiyo ni abiria 55 na wahudumu 7 wa ndege hiyo wakiwemo marubani. Aidha inasemekana hakuna aliyeokolewa na kwamba wote waliokuwemo wamepoteza maisha.325B842400000578-3499812-image-m-8_1458380499118

Leave A Reply