The House of Favourite Newspapers

Ndege ya Lion Air Indonesia Yaanguka Ikianza Kupaa Jakarta

NDENGE ya  abiria ya shirika la Lion Air aina ya Boeing 737 imeanguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege mjini Jakarta, maafisa wa Indonesia wamesema. Ndege hiyo safari nambari JT-610 iliyokuwa imewabeba abiria 188 ilikuwa safarini kutoka mji huo mkuu wa Indonesia kwenda Pangkal Pinang, jiji linalopatikana katika visiwa vya Bangka Belitung.

Baada ya kuruka iIitoweka kutoka kwenye mitambo ya rada saa kadhaa ilipokuwa inavuka bahari. Katika kikao na wanahabari, maafisa wamesema ndege hiyo, ambayo ni ndege mpya aina ya Boeing 737 MAX 8, ilikuwa imewabeba abiria 178 watu wazima, watoto watatu, marubani wawili na wahudumu watano wa ndege. Yusuf Latif, msemaji wa shirika la huduma za uokoaji na kuwatafuta manusura, amewaambia wanahabari na kuongeza: “Imethibitishwa kwamba ndege hiyo imeanguka.”Debris from Lion Air crashed plane

Afisa wa shirika hilo la ndege ameiambia BBC kwamba bado hawajui chanzo cha kuanguka kwa ndege hiyo. Afisa mkuu mtendaji Edward Sirait ameambia shirika la habari la Reuters: “Hatuwezi kusema chochote kwa sasa. Tunajaribu kutafuta maelezo na data zaidi.”

Vyombo vya habari Indonesia vimemnukuu afisa wa bandarini Tanjung Priok akisema kwamba maafisa wa boti la kusindikiza meli wameripoti kwamba wameona mabaki ya ndege hiyo kwenye maji.

Suyadi, ambaye hutumia jina moja pekee kama raia wengi wa Indonesia walivyo, amesema vyombo vingine vya baharini vimefunga safari kuelekea eneo hilo. Ndege hiyo safari namba JT-610 iliondoka Jakarta saa 06:20 saa za huko Jumatatu asubuhi (23:30 GMT Jumapili). Baada ya kusafiri kwa muda mfupi, ilitarajiwa kutua Pangkal Pinang saa moja baadaye.Indonesian Lion Air flight crash

Ndege hiyo inadaiwa kuwa Boeing 737 MAX 8, muundo wa ndege ambao umetumiwa kuanzia 2016. Tovuti ya kufuatilia safari za ndege ya Flightradar24 inasema ndege hiyo iliwasilishwa kwa Lion Air mwezi Agosti. Mtaalamu wa masuala ya uchukuzi wa ndege Gerry Soejatman ameambia BBC kwamba ndege hiyo  imekuwa ikikumbwa na hitilafu tangu ilipoanza kutumiwa, zaidi katika kupaa kwa utaratibu unaotakiwa.

Comments are closed.