The House of Favourite Newspapers

Ndege ya Mfalme Mswati Yazuiwa Canada

0

King Mswati

Mfalme wa Swaziland Mswati wa tatu akiwa na mmoja wa wake zake.

NDEGE binafsi ya Mfalme wa Swaziland Mswati wa tatu, imezuiwa nchini Canada kwa mara ya pili ndani ya miaka miwili kutokana na mzozo wa deni.

Ndege hiyo ilizuiwa kama sehemu ya kesi iliyo mahakamani, iliyowasilishwa na aliyekuwa mfanyibiashara mwenza wa mfalme Mswati raia wa Singapore Shanmuga Rethenam, ambaye anasema kuwa anaudai ufalme wa Swaziland kiasi cha dola milioni nane.

Jana Jumatano msemaji wa serikali ya Swaziland Percy Simelane, alikana madai kuwa mfalme ana deni lolote na kuongeza kuwa hatasema zaidi kwa kuwa kesi iko mahakamani.

Leave A Reply