The House of Favourite Newspapers

Ndege ya Misri Yatoweka Kwenye Rada na Abiria 69

0

EgyptAir
Ndege ya Shirika la EgyptAir la Misri ina ya Airbus A320 iliyotoweka kwenye rada.

Ndege ya Shirika la EgyptAir la Misri ina ya Airbus A320 ikitokea jijini Paris, Ufaransa kwenda Cairo, Misri imetoweka kwenye rada ikiwa na watu 69.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Shirika hilo, Airbus A320 ilitoweka katika maeneo ya mashariki ya Bahari ya Mediterranean, kilomita 16 kabla ya kufika katika anga la Misri.

Maofisa wanaosimamia safari za ndege wanasema kuwa ndege hiyo ilikuwa na abiria 59 na wahudumu 10.

Hakuna dalili zozote za kuwepo kwa hali mbaya ya anga zilizoripotiwa na nchi ya Misri imetuma ndege za kivita kuisaka ndege hiyo kwa ushirikiano na utawala wa Ugiriki.

Leave A Reply