The House of Favourite Newspapers

NDEGE YAANGUKA IKIJARIBU KUPAA

ABIRIA 50 wamenusurika kufa baada ya ndege waliyokuwa wamepanda kukosea njia na kudondoka katika eneo la Uwanja wa Wilson jijini Nairobi .

Imeripotiwa kuwa abiria na wafanyakazi kwenye ndege wameokolewa, baadhi wakiwa na majeraha, na wamekimbizwa hospitali na wanapatiwa matibabu.

Ndege hiyo ya kampuni ya Silverstone Air ilikuwa ikifanya safari kuelekea kuelekea Malindi nchini Kenya, na wakati inajaribu kuruka, ilipoteza muelekeo na kuanguka.

Comments are closed.