The House of Favourite Newspapers

28 Wafariki Ndege Ikianguka Kwenye Makazi ya Watu

WATU ishirini na nane wamefariki mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kutokana na ajali ya ndege iliyoanguka katika eneo la makazi ya watu ambapo 10 miongoni mwao ni wakazi wa eneo husika.

 

Ndege hiyo ilianguka katika mji wa Goma, mtaa wa Birere, karibu na mpaka wa Congo na Rwanda.

 

Vyombo vya usalama vinaendelea na uchunguzi ili kufahamu idadi halisi  ya walikufa na waliojeruhiwa. Zoezi hilo linafanyika kwa msaada wa wananchi wa mji huo ambao wanaendelea kupekua nyumba za majirani zilizoangukiwa na ndege hiyo ya kampuni ya Beesyby.

 

Kampuni hiyo imekuwa ikifanya safari zake huko Kivu kaskazini ikisafiri kati ya miji ya Goma, Butembo na Beni.

 

Waziri wa Afya wa Kivu, Kakule Kanyere Moise,  anasema kwa sasa ni mapema mno kutaja kwa uhalisi idadi ya watu waliofariki na waliojeruhiwa.

Comments are closed.