The House of Favourite Newspapers

Ndege Yachomoka Gurudumu, Yashuka kwa Dharura

NDEGE ya Shirika la Silverstone imelazimika kutua kwa dharura baada ya gurudumu lake kuanguka wakati ikipaa, jana Jumatatu, Oktoba 28, 2019.

 

Ndege hiyo aina ya Dash 8 – 300 iliyokuwa ikitokea Lodwar kwenda Nairobi ililazimika kutua katika Uwanja wa Kimataifa wa Eldoret jijini Nairobi nchini Kenyawakati ikiwa imebeba abiria wanne ambao walikuwa wakisafiri kutoka Lodwar kuelekea Jijini Nairobi.

 

Abiria wote wamesalimika na kutafutiwa usafiri mwingine wa ndege ya shirika la Skyward iliyowapeleka hadi Nairobi.

 

Inaelezwa kuwa, Octoba 11, mwaka huu, ndege hiyo ililazimika kutua baada ya kupoteza mwelekeo wakati ikitokea Nairobi kwenda Lamu.

 

Comments are closed.