The House of Favourite Newspapers

Ndege Yatekwa Nyara Nchini Libya, Yatua Malta

ndege-imetekwa-libya-malta-1

MALTA: Ndege moja ya abiria ya nchini Libya imeripotiwa kutekwa nyara leo Ijumaa, Desemba 23, 2016, ikiwa kwenye safari kutokea Mji wa Sabha ulioko Kusini Magharibi mwa Libya, kuelekea mjini Tripoli kabla ya kubadili uelekeo na kutua nchini Malta.

ndege-imetekwa-libya-malta-2Ndege hiyo aina ya Airbus A320, mali ya Shirika la Ndege la Serikali ya Libya, Afriqiyah, ilikuwa na abiria 118 ambapo 111 ni abiria na wengine 7 ni wafanyakazi wa ndege hiyo, wakati ikitekwa huku watekaji nyara wawiili wakiripotiwa kutekeleza tukio hilo na kutishia kuilipua ndege hiyo.

ndege-imetekwa-libya-malta-4Waziri Mkuu wa Malta, Joseph Muscat ameeleza kuwa, mpaka sasa takribani abiria wote wameokolewa na Kikosi Maalum cha Usalama cha nchini mwake ambapo jumla ya watu 109 wameshaachiliwa.ndege-imetekwa-libya-malta-3

Hizi ni baadhi ya Tweet zake.

Kamanda Mpinga; Madereva Zaidi ya 280 Tayari Tumewafikisha Mahakamani

Updates

Comments are closed.