TCAA Yafuta Kibali Ndege za Kenya Kutua Tanzania

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imefuta kibali kilichokuwa kikiruhusu ndege za Shirika la Ndege la Kenya (KQ) kutua Tanzania, uamuzi huo umekuja baada ya Kenya kutoijumuisha Tanzania katika orodha ya Nchi ambazo Raia wake wataruhusiwa kuingia Kenya kuanzia Agosti 01.

 

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Kenya kutoa orodha ya nchi ambazo raia wao wataruhusiwa kuingia nchini humo kwa ndege kuanzia kesho watapofungua mipaka yao ya kimataifa.

 

Orodha hiyo haikuwataja Watanzania hivyo kupelekea Tanzania ambayo ilikuwa inaruhusu ndege za Kenya kuingia nchini kusitisha (nullify) ruhusa hiyo.

 

Ndege za Kenya hazitoruhusiwa kutua katika uwanja wa ndege wa JNIA – Dar es Salaam, KIA – Kilimanjaro, wala AAKIA – Zanzibar.

 

Kenya imetangaza kufungua anga lake kuanzia kesho, baada ya kulifunga kwa zaidi ya miezi minne ili kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.

Toa comment