The House of Favourite Newspapers

Ndikumana Amkumbuka Uwoya

MANYUNYU ya mvua yanaulowesha mwili wangu, baridi kali inapenya vilivyo kwani sikuwa na koti. Eneo nililopo lina utulivu wa hali ya juu, chini ya mti naona kuna mabaki ya magogo yaliyoungua.

Najaribu kuvuta picha nipo sehemu gani, akili inakataa. Sijui nipo sehemu gani. Nasikia mlio wa mnyama nisiyemjua kwa mbali. Najaribu kufikicha macho ili nione vizuri, ghafla nasikia sauti nyuma yangu.

 

Ni sauti yenye lafudhi ya Kinyarwanda, nageuka na kumtambua kuwa ni yule kocha wa Timu ya Rayon Sports na aliyekuwa mume wa muigizaji wa sinema za Kibongo, Hamad Ndikumana.

Haraka sana natoa kalamu na note book yangu ili niweze kufanya naye mahojiano:

MIMI: Habari za siku, mzima wewe?

NDIKU: Mimi sijambo habari za huko utokako? Nakukumbuka wewe kijana uliwahi kunisumbua sana kwa kufuatilia habari zangu.

MIMI: Hahaha ni kweli kaka, unajua ni kazi yetu hii ndio inanifanya niwe msumbufu lakini ukinikuta kwenye maisha ya kawaida, mimi mpole sana. Uliondoka ghafla sana, unaweza kutuambia ilikuwaje?

NDIKU: Daah ata sielewi lakini nakumbuka tu nilikuwa nmetoka kwenye mazoezi ya timu yangu, nikajikuta tu nipo huku. Vipi lakini Uwoya yupo? Niliacha anatembea nasikia na Dogo Janja, kuna ukweli wowote?

 

MIMI: Daah hapo kwa kweli sina uhakika sana maana Uwoya haaminiki na unaweza kuta ni kweli anatoka naye lakini suala la ndoa ndio ambalo siliamini asilani.

NDIKU: Ila warembo wa Bongo Movies nawakumbuka sana, Johari yupo? Bado anaendelea kupiga ulabu kama kawa?

MIMI: Hahaha Johari yupo, hata yeye huwa anakukumbuka sana. Anakumbuka zile bata ulizokuwa unawapa wakati ule mambo yalivyokuwa mazuri. Kuhusu mtungi kwa sasa ametangaza kuacha japo siwezi kumwekea dhamana juu ya hilo. Ya Mungu mengi, unaweza mnasa siku anapiga kama kawa.

NDIKU: Hivi bado Johari yupo na Ray wake? Wanaendeleaje lakini?

 

MIMI: Mapenzi yalishaisha zamani. Sasa hivi wanapiga kazi tu pamoja ingawa ni muda mrefu sasa hatujaona kazi kutoka katika kampuni yao.

NDIKU: Nini tatizo? Au Watanzania hawataki tena kutazama muvi zao?

MIMI: Sidhani, kuna mabadiliko tu ya kiutawala ambayo yameathiri vitu vingi. Wale mafisadi waliokuwa wanamwaga hela mtaani sasa hivi hawatoi tena hivyo hata wale ndugu zao waliokuwa wananunua filamu, kwa sasa wamepungua kidogo.

NDIKU: Unataka kuniambia hiyo ni sababu ya wao kutofanya vizuri?

MIMI: Hiyo ni moja wapo lakini nyingine ni wao wenyewe. Wamekosa ubunifu hivyo wanajikuta wakishindwa kupambana na hali ngumu ya uchumi na kuwashawishi watu wanunue kazi zao.

 

NDIKU: Hayo mambo ya kutegemea mafisadi nilikuwa siyapendi. Nilikuwa nayaona sana kwa wasanii haswa wa Bongo Movies. Walikuwa hawajitumi, walikuwa wanategemea sana matajiri ndio wawape fedha na kufanya maonesho kwamba wana fedha kumbe wala si zao.

Matokeo yake sasa ndio hayo. Msingi wao ungekuwa kwenye kazi, hata sasa hivi ingekuwa rahisi wao kutoboa lakini ndio hivyo unaniambia wapo juu ya mawe.

MIMI: Ni kweli kabisa. Nitauchapisha ujumbe huu kwenye magazeti yetu ya Global Publisher ili waweze kujifunza pia.

NDIKU: Sawa tu, itakuwa vizuri. Nani sasa anafanya vizuri kwa sasa kwenye gemu la Bongo Movie?

 

MIMI: Siku hizi wengi wamekimbilia kwenye tamthiliya, angalau wameona huko kunalipalipa. Wanapiga pesa kutoka kwenye makampuni yanayorushwa tamthiliya zao kwenye ving’amuzi mbalimbali.

NDIKU: Uwoya ana biashara gani lakini mjini maana natamani nikimuona anafanya kazi angalau apate fedha na amtunze na mwanangu vizuri.

MIMI: Hilo nadhani analimudu kwa namna anayoijua yeye maana namuona mtoto anasoma shule nzuri. Kuhusu biashara, alifungua baa ikafanya vizuri lakini juzikati ilisimama kwa muda ila nimeambiwa ameifufua tena. Inaendelea kutoa huduma kama kawaida pale Sinza-Mori.

NDIKU: Vipi Imelda Mtema yupo? Yule alikuwa msaada mkubwa sana wakati ndoa yangu na Uwoya ilipokuwa inasuasua, alikuwa anaripoti wakati mwingine ilikuwa inanisaidia.

 

MIMI: Yupo, amejaa tele. Anaendelea na upaparazi kama kawa.

Ndiku: Poa bwana, acha mimi nisepe nakwenda kumuona Kanumba pale aliniambia ana uzinduzi wa filamu.

Wakati nataka kumjibu, ghafla nashtuka na kujiona nipo kitandani kwangu na kugundua kuwa nilikuwa naota. Ndoto hizi jamani!

Na Erick Evarist | SAA TISA USIKU KITANDANI kwangu

Comments are closed.