Ndoa ya Ben Pol, Anerlisa palepale

 

Baada ya uvumi wa maneno ya waja kuhusu mastaa kuchumbia au kuchumbiwa na kuacha au kuachwa solemba, mwanamuziki wa RnB Bongo, Benard Paul ‘Ben Pol’ amevunja ukimya.

 

Baada ya kumchumbia mrembo tajiri kutoka nchini Kenya, Anerlisa Muigai, wengi walitarajia kuwa kilichokuwa kinafuata ni ndoa kati ya Ben Pol na mrembo huyo, lakini miezi ikawa inakatika tu huku baadhi ya wananzengo wakidai uchumba huo umevunjika.

Katika mahojiano maalum na Gazeti la Ijumaa, mapema wiki hii, Ben Pol alieleza kuwa mipango ya ndoa iko palepale. Alisema suala hilo ni la kifamilia zaidi hivyo mashabiki wake wasisikilize maneno ya watu, bali wasubiri waone nini kitakachofuata.

“Unajua kuna kitu watu wanachanganya, mambo ya ndoa ni ya familia zaidi, siyo kila kitu unatakiwa kukiweka wazi. “Kwa hiyo, watu watulie ili waone nini kitatokea na kama ikitokea, muda ukifika wataona tu kwa sababu ndoa siyo jambo la siri na lazima kabla ya hapo watu watapata taarifa tu.

“Kwa sasa ninaweka mambo fulani sawa, lakini ndoa iko palepale. “Kwa upande wa kazi yangu ya muziki nimeachia wimbo mpya wiki mbili zilizopita unaitwa Sana. “Wimbo huo nimemshirikisha mwanamuziki wa Nigeria anaitwa Timaya kwa sababu nilikaa muda mrefu kama miezi saba au nane bila kutoa wimbo kwa hiyo sasa ninalipiza kwa kutoa wimbo kila mwezi hadi Desemba. “Naomba mashabiki wangu waendelee kunisapoti kwenye kazi zangu,” alisema Ben Pol.

Stori: NEEMA ADRIAN,Ijumaa

Toa comment