The House of Favourite Newspapers

NDOA YA CHAZ BABA VISA VYAANZA!

Charles Gabriel ‘Chaz Baba

DAR ES SALAAM: Chokochoko! Takriban wiki moja baada ya kufungwa kisha kufuatiwa na sherehe kabambe kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, ndoa ya mwanamuzki wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’, tayari visa vimeanza, Ijumaa limedokezwa.  Wiki iliyopita Chaz Baba alifunga ndoa kwa mara nyingine na mwanamke aitwaye Mariam. Katika ndoa hiyo visa vimeanza baada ya mzazi mwenza wa Chaz Baba ambaye ni msanii wa Bongo Muvi, Husna Idd ‘Sajenti’ kujitokeza na kusema kuwa anachojua jamaa huyo ataoa sana, lakini mke halali aliyepangiwa na Mungu ni yeye.

Katika mazungumzo na Gazeti la Ijumaa, Sajenti alisema kuwa, Chaz Baba ni baba wa mtoto wake wa kwanza na anaamini kuwa hawezi kudumu na Mariam kwani atakuja kuwa mumewe kabisa baadaye. Sajenti alisema hata kama Chaz Baba amefunga ndoa hiyo haimpi shida kwani anajua tu atarudi kwake ili wamlee mtoto wao.

“Najua Chaz ni wangu, kwani unajua zimepita ndoa ngapi kwake? Ndoa itakayodumu ni ile atakayofunga na mimi, hicho ndicho ninachokijua hadi ninaingia kaburini, asijidanganye, hawezi kudumu na huyo mwanamke (Mariam),” alisema Sajenti akionekana mwenye hasira.

Baada ya kumsikia Sajenti, Ijumaa lilimtafuta Chaz Baba ambapo alifikishiwa kauli ya mzazi mwenzake huyo na kutakiwa kutia japo neno, lakini mwenyewe aliishia kucheka na kusema kuwa duniani kuna mambo sana hivyo lazima acheke. “Duniani kuna mambo sana, acha nicheke tu, acha tuone maana mimi sitii neno,” alisema Chaz Baba. Kabla ya kufunga ndoa na Mariam, mwaka 2013, Chaz Baba alifunga ndoa na mwanamke mwingine kabla ya kuachana miaka michache baadaye.

Comments are closed.