The House of Favourite Newspapers

NDOA YA KINYAIYA, KAPUYA…NANI ANATESEKA ?

DAR ES SALAAM: Gumzo la aina yake limeibuka mitandaoni baada ya picha ya ndoa ya Waziri wa Zamani wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Profesa Juma Kapuya na mtangazaji maarufu Bongo, Benny Kinyaiya kuzagaa, Risasi Mchnaganyiko linakuhabarisha.  

 

Kila zilipotupiwa picha hizo kwenye kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii hivi karibuni, watu ilikuwa full kukomenti hadi wengine wakaulizana kwani nani anateseka na ndoa hizo? “Siamini; Benny kaoa kweli au anatufanyia sanaa za maigizo?” Posti moja ilisomeka kwenye Mtandao wa Instagram ikiambatanishwa na picha inayodaiwa ni ya ndoa ya Benny na mkewe ambaye hakufahamika jina.

 

Komenti nyingine hazina mashiko ya kuandikwa kwenye gazeti, lakini hivi karibuni mwandishi wetu aliibuka kwenye sherehe iliyodaiwa kuwa ni ya harusi ya Benny iliyofanyika eneo la Ilala-Boma jijini Dar, lakini alizuiliwa na walinzi kuchukua matukio kwa hoja kwamba hafla hiyo haikutakiwa kujulikana kwenye jamii.

 

Hata hivyo, mambo yaliendelea kuwa moto mitandaoni na picha ya ndoa iliyosambazwa na asiyejulikana ilizidi kujichukulia umaarufu kwa watu kuitumia na kuandika watakayo.

 

Lakini hoja kubwa ilikuwa ni kwamba mwanamke huyo aliyetajwa kuwa na fedha nyingi alikuwa amemnunulia gari la kutanulia maisha Benny. Maelezo ya wachangiaji wengi mitandaoni hayakuweza kufika mwisho wa hoja kwamba mwanamke huyo kuwa na fedha kunabeba taswira gani kwa yeye kuolewa na Benny.

HUYU HAPA BENNY

Lakini kama ujuavyo kazi ya mwandishi ni kufungua ishu zilizofungwafungwa, Benny alitafutwa ili ajibu hoja za kununuliwa gari na mwanamke huyo, kufunga ndoa ya maigizo, jina la mke wake na makazi yake ni wapi? Msikilize Benny akijibu maswali kama alivyoulizwa na mwandishi wetu; utakachoambulia ndicho mwandishi wetu alichojibiwa.

 

Risasi: Maneno yapo mengi mitandaoni, wapo wanaosema umefuata pesa, wengine umepewa gari na wengine ni filamu…

Benny: Sasa wewe ulitaka kujua nini?

RISASI: Utufafanulie kama ni ndoa kweli haina shaka?

 

BENNY: Unajua vitu vingine ni vya watu binafsi, hivi ni vitu vingine kama wewe (mwandishi) ulivyo na mkeo kuna vitu hutaki vitoke nje. Sasa wanaosema ndoa siyo ndoa hayo yanatoka wapi? Mimi nina magari wewe mwandishi unanijua, nina magari mawili matatu…mawili matatu.

Hela ninayo, hao wanaosema hayo maneno mimi nawaangalia ndiyo maana nimekaa kimya vitu vingine vya ndani havipaswi kutoka nje.

RISASI: Tunasikia shemeji makazi yake ni Uingereza…

BENNY: Haa haa! Hayo ni mambo ya ndani (anacheka) mimi maisha yangu siyo ya wasiwasi, nina kila kitu kijana wa miaka yangu anatakiwa kuwa nacho. Hakuna chochote wala sijui chochote kama unavyosema sijui makazi yake kama ni Uingereza.

Risasi: Labda unipe jina nipate kumjua shemeji yangu!

Benny: Jina lake? Haaa haa kwani wewe unajua ni shemeji yako tayari? Hayo ni mambo ya ndani mwandishi! Haa haaa, baadaye watu watataarifiwa kama kuna kitu chochote. Nitasema tu mimi ni mtu wa watu.

 

Risasi: Lakini umekuwa ukifuatiliwa sana kutokana na ndoa yako hii?

Benny: Yaani imekuwa ni tabu, sikai, nikalala kuanzia asubuhi hadi asubuhi kwa siku simu mia mbili hadi mia tatu. Yaani napata shida sijawahi kuona. Baadaye watu watajua kweli kama kuna kitu chochote kinachoendelea!

 

Risasi: Kwa hiyo honeymoon kaka ipo wapi sasa?

Benny: Hakuna kitu, hakuna kitu mwandishi!

Risasi: Nilitaka kujua mtakuwa honeymoon wapi nije kupata japo soda na shemeji yangu!

Benny: Hakuna chochote pale ilikuwa get together ya familia kukiwa na chochote nitakujulisha wewe mtu wangu.

MARA PAAP!

Wakati Benny akimaliza mahojiano na kuuacha utata wa ndoa yake uendelee na watu wadadisi wapendavyo, mara paaap picha ya Profesa Kapuya ikashika kasi mitandaoni.

 

“Mzee naona kaopoa kitu kipyaaa.” Posti moja iliwekwa kwenye mtandao wa Fecebook ikiambatanishwa na picha ya ndoa ya Profesa Kapuya. Gazeti hili lilipofuatilia ukweli wa ndoa hiyo lilibaini kuwa waziri huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 73 alikuwa amefunga ndoa huko Urambo mkoani Tabora kwa kumuoa Mwajuma Mwitiko (25).

 

Unajua tena maneno ya waja, walianza kusema kwamba waziri huyo wa zamani ambaye ni mpenzi kindakindaki wa Simba alikuwa amepita mulemule wanapopita wazee wenzake wengi kwa kupenda kuoa wanawake ‘wabichi’ kwelikweli. Hata hivyo, gazeti hili linapenda kumpongeza mzee Kapuya kwa kuweza kufunga ndoa na linamuomba Mungu aifanye ndoa hiyo kuwa ya heri na baraka tele.

 

Aidha linamuomba Benny kuweka wazi ukweli wa ndoa yake kwa badala ya kuendelea kufanya siri kwa sababu ndoa ni jambo la heri ambalo linatakiwa kufurahiwa na watu wengi wakiwemo ndugu, jamaa na marafiki zake na hasa ukizingatia kuwa yeye amekuwa staa hapa Bongo kwa muda mrefu.

Comments are closed.