The House of Favourite Newspapers

NDOA YA MWANAHERI YAKWAA SKENDO No.1

 

MAMBO ni moto! Saa chache baada kufungwa, ndoa ya kimyakimya ya staa wa Bongo Movies na Tamthiliya, Mwanaheri Ahmed ‘Mwana’ imekwaa skendo namba moja baada ya kuanza kupigwa zengwe kwamba eti ameolewa mke wa pili.

 

TUJIUNGE NA CHANZO

Kwa mujibu wa chanzo makini cha Gazeti la Ijumaa Wikienda ambacho ni mtu wa karibu wa familia ya Mwanaheri, mwanaume huyo aliyemuoa anajulikana kwa jina moja la Khamis ambaye ni mfanyabiashara maarufu na tayari ana mke mwingine na watoto.

 

Ilidaiwa kuwa, ndiyo maana mwanaume alifanya tukio hilo kwa siri kubwa bila mkewe kujua ndiyo maana hata baadhi ya rafiki zake Mwanaheri hawakualikwa.

Chanzo hicho kiliendelea kumwaga ubuyu kwamba, mipango hiyo ya ndoa ilifanywa na watu wachache mno.

 

“Kama hamna ubuyu kamili ni kwamba mwanaume aliyemuoa Mwanaheri ana mke wa ndoa na watoto. Ndiyo maana ameamua kufanya ndoa hii kuwa ya kimyakimya bila watu wengi kujua.

“Kingine ambacho watu hawakijui ni kwamba, huyo mwanaume aliyemuoa Mwanaheri amemzidi umri kwa kiasi kikubwa,” kilitiririka chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa gazetini.

 

MWANAHERI NA IJUMAA WIKIENDA

Kama ilivyo desturi ya Ijumaa Wikienda, mara baada ya kunyetishiwa skendo hiyo ambayo ndiyo habari ya mjini, lilimtafuta Mwanaheri ili afunguke anachokijua juu ya hoja hizo mbili- kuwa ni mume wa mtu na kwamba amemzidi umri mno ambapo mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo;

Ijumaa Wikienda: Mambo vipi Mwanaheri? Mbona umekula harusi mwenywe, kulikoni?

Mwanaheri: Sijala mwenyewe jamani…ilikuwa ya harakaharaka.

Ijumaa Wikienda: Kwa nini ikawa ya harakaharaka?

Mwanaheri: Basi tu, mume wangu alikuwa na safari ya ghafla ndiyo maana shughuli ikawa ya ghaflaghafla.

 

Ijumaa Wikienda: Mbona kuna taarifa kuwa huyo mwanaume aliyekuoa ni mume wa mtu na ana watoto?

Mwanaheri: Hapana… siyo kweli kabisa…mimi ninachojua ana watoto tu basi…

Ijumaa Wikienda: Sasa kwa nini ulikuwa unamficha asionekane kwenye picha za tukio lenu la kufunga ndoa hadi Ijumaa Wikienda likatumia nguvu ya ziada kupata picha zake?

Mwanaheri: Ni uamuzi wa mtu, unajua hapendi kufahamika kwa watu.

Ijumaa Wikienda: Pia inadaiwa kuwa unamficha kwa sababu amekupita umri kwa miaka mingi, yaani ni sawa na baba yako, je, unazungumziaje hilo?

 

Mwanaheri: Mimi nilichoangalia ni ndoa tu na stara yangu, lakini siyo kitu kingine.

Ijumaa Wikienda: Kwa hiyo inawezekana akawa kweli ni mume wa mtu kutokana na umri alionao?

Mwanaheri: Hapana, umri siyo kigezo kinachoweza kuonesha kuwa mtu ameoa maana inawezekana amechelewa kwa sababu zake binafsi.

Ijumaa Wikienda: Poa Mwanaheri.

Mwanaheri: Poa karibu sana.

 

IJUMAA WIKIENDA LASAKA RIPOTI KAMILI

Kufuatia skendo hiyo kuwa gumzo, kumekuwa na mengi yanayosema juu ya ndoa hiyo hivyo Gazeti la Ijumaa Wikienda lipo mitaani kusaka ubuyu kamili ili kuurusha hapahapa.

Stori: Imelda Mtema, Dar

Comments are closed.