NDOA YA NELLY KAMWELU YANUKIA

Nelly Kamwelu

NDOA ya Miss Universe Tanzania na Miss Southern Africa Interna­tional 2011, Nelly Kamwelu inanukia baada ya taratibu za awali kuanza kufanyika huku ikielezwa kuwa, anayemuoa ni mwanaume ambaye wame­kuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu.  Akizun­gumza na Ijumaa Wikienda, Nelly alisema kuwa anamshukuru Mungu ameweza kumpata mtu ambaye anam­penda na anaahidi kuwa mke bora baada ya tukio hilo la heri kukamilika.

“Unajua kila jambo na wakati wake, yamesemwa mengi juu yangu lakini nashukuru Mungu siku si nyingi nitaandi­ka historia katika mai­sha yangu, kwa lugha nyingine ni kwamba naolewa ‘soon’ kwani nimeshachumbiwa,” alisema Nelly.

STORI: Imelda Mtema, Ijumaa Wikienda

Loading...

Toa comment