NDOA YA SHAMSA KUVUNJIKA KISA MTOTO?

Shamsa Ford

MWIGIZAJI bomba wa Bongo Muvi, Shamsa Ford amewajibu wanaomsema kwamba ameshindwa kumzalia mume wake, Chid Mapenzi mtoto na kwamba ndoa si mtoto na kila mtu ana mipango yake ya kuzaa baada ya ndoa, hivyo waache kuongea wasiyoyajua.  Kwa mujibu wa Shamsa, kila ndoa ina mipango hasa katika suala la kupata mtoto kwani kuna wengine wanapanga kuzaa hata baada ya miaka mitano hivyo hata yeye na mume wake wana mipango yao ya ndani ya ndoa hivyo pale Mwenyezi Mungu atakapowabariki watapata mtoto.

“Kikubwa ambacho ninaweza kuwaambia watu ni kwamba tuombeane mema kwa kuwa maisha ni mafupi na hakuna anayeujua mwisho wake na hata katika dini, Mungu amesema kwamba ukimuombea mwezio mema na wewe utabarikiwa zaidi,” alisema Shamsa na kuongeza: “Hivyo kama kuna mtu ambaye hajaolewa na ananiombea mimi niachane na mume wangu, basi ni boraawe makini kwa kuwa yeye anaweza akakosa hata mume wa kumuoa kwa kuniombea mimi mabaya.”

Hata hivyo, Shamsa alimalizia kwa kusema kwamba siku ya harusi yao kuna watu walidhani kwamba ataachana na Chid Mapenzi baada ya muda mfupi, lakini kwa uwezo wa Mungu mpaka sasa ni mwaka wa tatu na bado wapo pamoja hivyo anaamini kwamba talaka si jambo jema kidini na Mungu hawezi kuruhusu ndoa yao ivunjike na kama ikivunjika, basi anaamini itakuwa ni mipango ya Mungu.

Stori: MWANDISHI WETU, IJUMAA


Loading...

Toa comment