Ndoa ya ughaibuni yamshinda Richa Adhia

richa5

Miss Tanzania 2007, Richa Adhia.

Stori: Imelda Mtema

VUNJA ukimya! Miss Tanzania 2007, Richa Adhia ambaye amevunja rekodi kwa kutokuwa na skendo tangu anyakue taji hilo, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusiana na ndoa yake ambayo alikuwa akitarajia kuifunga ughaibuni na mchumba wake wa muda mrefu, Hridhaan Dhllon.

Akizungumza na gazeti hili, Richa alisema kuwa kila kitu kilienda sawa lakini kukawa na kikwazo kimoja kikubwa cha yeye baada ya kufunga ndoa kwenda kuishi nje na mumewe,

jambo ambalo lilikuwa gumu kwake. “Taratibu zote zilikamilika lakini tulishindwana sehemu ya kuishi.Yeye alitaka tukaishi nje lakini ilishindikana hivyo na ndoa ikayeyuka, tumebaki marafiki tu wa kawaida,” alisema Richa.

Loading...

Toa comment