The House of Favourite Newspapers

NDOA ZA MASTAA HAWA…ZIMEFUNGWA ,KUVUNJIKA KWA MWENDOKASI!

Image result for NDOA YA NUH NA NAWAL

MAISHA ya ndoa kwa mastaa yamekuwa na changamoto nyingi huku wengi wao wakitajwa kuingiza sanaa kwenye ndoa zao hivyo kujikuta zikishindwa kudumu.  

 

Japo ukweli ni kwamba zipo pia ndoa watu wa kawaida ambazo zimekuwa zikivunjika lakini za mastaa zimekuwa zikionekana zaidi kutokana na kwamba wao ni kioo cha jamii na kila mtu anawatazama.

 

Bahati mbaya sana, inaonekana, zipo ndoa za mastaa ambazo wahusika waliingia harakaraka yaani zile za kuwa kwenye uchumba kwa muda mfupi na baada ya siku chache kuoana na ndizo hizohizo baada ya miezi kadhaa (mwendokasi) au mwaka zimevunjika. Katika makala haya tunakuletea listi ya mastaa ambao waliingia kwenye ndoa za chapchap, lakini zikadumu kwa muda mfupi kisha kuvunjika.

 

DOGO JANJA NA UWOYA

Wakati mwanamuziki Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ na msanii wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya wanafunga ndoa ilionekana kuwa kama ni kiki kwa sababu ndoa hiyo wazazi wa pande zote mbili hawakuhudhuria hivyo kuwaweka wasanii wenzao kuchukua nafasi za wazazi.

Image result for NDOA YA DOGO JANJA NA UWOYA

Baadaye siku zilivyosonga mbele wawili hao walikiri kwamba ni ndoa ya kweli na wakawa wanaishi pamoja kama mume na mke lakini baada figisu zilianza. Ndoa ya wawili hao imedumu kwa mwaka mmoja kwani ilifungwa Oktoba mwaka 2017 na hivi karibuni ilidaiwa kuvunjika kwa kile kilichodaiwa ni usaliti.

 

SKAINA NA SAAD

Muigizaji Skyner Ally ‘Skaina’, yenye aliingia kwenye ndoa mwaka 2011 na kijana anayeitwa Saad Omar, ambapo ndoa hiyo ilivunjika baada ya siku nne wakiwa mapumzikoni ‘Honeymoon’ huku kisa kikiwa mwanaume kugundua kuwa msanii huyo alikuwa na ujauzito wa miezi mitano ambao haukuwa wake.

Image result for NDOA YA WASTARA NA SADIFA

WASTARA NA SADIFA

Msanii huyu wa filamu Wastara Juma na Mbunge wa Donge, Zanzibar, Sadifa Khamis Juma walifunga ndoa ya kimyakimya tena ya harakaharaka ambayo ilihudhuriwa na ndugu wa karibu tu.

Ndoa hiyo ilifungwa Januari 7, 2016 ambapo ilidumu kwa miezi miwili na siku kadhaa na kuvunjika ambapo mwenyewe alidai kwamba aliamua kuondoka kutokana na kuwa hakuwa na furaha ya ndoa kwani mumewe alikuwa akimfanyia mambo ambayo hayakupendeza kwani kabla ya ndoa aliahidiwa vitu vingi lakini mbunge huyo hakuvitekeleza.Image result for NDOA YA MENINAH NA ABDULKARIM

MENINAH NA ABDULKARIM

MWANAMAMA huyu ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, Meninah Atick mwaka 2015 alifunga ndoa na mtoto wa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Abdukarim Haule lakini ndoa hiyo haikuweza kudumu. June 6, 2016 muimbaji huyo alitangaza kuingia tena kwenye maisha ya ndoa na mwanaume mwingine ambaye hakumuweka wazi jina lake.

Image result for NDOA YA SABBY NA JARUF

SABBY NA JARUF

Mrembo huyu kutoka kwanye kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva na filamu, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ aliolewa ndoa ya kimyakimya na mwanaume Mwarabu aliyefahamika kwa jina la Jaruf. Baada ya kuolewa, alidumu kwenye ndoa hiyo kwa siku saba tu na kuvunjika alisema alishindwa kuendelea kutokana na tabia za waarabu, licha ya kuachika hapo alidaiwa kuendelea kuolewa na kuachika zaidi ya mara tatu.

 

NUH MZIWANDA NA NAWAL

Mbongo Fleva, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii mwenzake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ lakini wakati wakiendelea na mapenzi yao ghafla mwanamuziki huyo akafunga ndoa ya harakahaka na Nawal.

 

Kwa mujibu wa Nuh alifunga ndoa hiyo kwa sababu Nawal alikuwa na ujauzito wake hivyo wazazi kumtaka afanye hivyo ambapo alibadili dini na kufunga ndoa ya Kiislamu ambayo ilidumu kwa miezi tisa tu na kuvunjika wakiwa wamejaliwa mtoto mmoja wa kike.

Image result for NDOA YA KARAMA NA AISHA

KARAMA NA AISHA

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Luteni Karama aliingia kwenye ndoa na Aisha Yassin ambapo nayo ilidumu kwa miezi 10 na kuvunjika. Karama alifunga ndoa ya siri na ya harakaharaka kwani alikuwa ndani ya uhusiano wa kimapenzi na msanii mwenzake, Isabela Mpanda ambapo Aisha alikuwa rafiki wa Isabela lakini ndoa hiyo haikuweza kudumu.

Comments are closed.