The House of Favourite Newspapers

Ndonga za Global TV… Balozi wa Malawi Mgeni Rasmi

0
Balozi wa Malawi nchini, Hawa Ndilowe.

 

BALOZI wa Malawi nchini, Hawa Ndilowe anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Mapambano ya Ubingwa wa Global TV, Afrika Mashariki na Kati yatakayopigwa kesho Jumapili kwenye Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar.

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania, (TPBO) Yassin Abdallah ‘Ustaadh’ alisema balozi huyo wa Malawi amekubali kuwa mgeni rasmi katika pambano hilo ambalo litaambatana na burudani ya Muziki wa Bongo Fleva.

 

“Mabondia wanatarajia kupima uzito leo Jumamosi kwa ajili ya ndonga za kuwania ubingwa wa Global TV, lakini kikubwa ni kwamba Balozi wa Malawi amekubali mwaliko wa kuwa mgeni rasmi pia atakuwa akitoa sapoti kwa kijana wake, Israel Kamwamba atakayezichapa na Francis Miyeyusho.

 

“Kitu kingine kikubwa ni kuwa kamati imepokea maombi ya wadau kutaka kuja ukumbini sasa tumekubali kuweka kiingilio cha Sh.5,000 pekee kwa sababu suala la kurusha live lipo kama lilivyo na tunategemea kuwa na wasanii wa Bongo Fleva kwa ajili ya kutoa burudani ambao ni Pam D, Wakali Dancers, Snura, Mr Dox na Dalada,” alisema Ustaadh.

 

Wakati huohuo jana mabondia hao walitambulishwa kwa waandishi wa habari tayari kwa kuzichapa hapo kesho saa 2 usiku. HII SI YA KUKOSA KABISA MTU WANGU!

STORI: IBRAHIM MUSSA | RISASI JUMAMOSI

Leave A Reply