The House of Favourite Newspapers

BREAKING: Ndugai Amwapisha Mtaturu Kumrithi Lissu – Video

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, amemwapisha Miraji Mtaturu kuwa Mbunge wa Singida Mashariki (CCM), leo Jumanne Septemba 3, 2019, bungeni jijini Dodoma akichukua nafasi ya Tundu Lissu ambaye ubunge wake ulifutwa Juni 28, 2018 baada ya kupoteza sifa za kuendelea kuwa mbunge.

 

Baada ya Miraji kuapishwa, Ndugai amesema kuwa, sasa watu wa Singida Mashariki wanaye mwakilishi halisi bungeni.

 

Aidha, wakati Mtaturu akiapishwa, wabunge wa upinzani wamesusia tukio hilo kwa kugoma kuingia ukumbini katika kipindi hiki cha asubuhi.

 

TAZAMA VIDEO HAPA

Comments are closed.