Ndugu Wawili Wakaa Baharini Siku 21, Waokotwa

RAIA wawili wa Comoro wameokotwa katika bahari ya Hindi ukanda wa Msuka Wilayani Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba wakiwa na chombo chao cha  uvuvi baada ya kukaa baharini wa muda wa siku 21.

 

Wavuvi hao ambao ni ndugu wa familia moja wameokotwa  na wavuvi muda wa saa tano usiku wa kuamkia juzi na wamefikishwa katika hospitali ya Wete Visiwani humo kwa ajili ya kupatiwa huduma ya kwanza.

 

Akizungumza kwenye eneo la tukio, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba- Zanzibar, Salama Mbarouk amesema tayari wamekabidhi Idara ya Uhamiaji kwa hatua na taratibu za kuwarejesha nchini kwao.

 

Mrakibu Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Pemba,  Said Mussa Khamis  amesema wanaendelea na taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwapatia huduma na mahitaji ya kibinadamu.

 

Naye kaimu Daktari wa hospitali ya Wete walikofikishwa wahanga hao alisema wanaendelea kuwapa huduma za kinga dhidi ya maradhi ya baadaye baada ya kukaa siku nyingi baharini.

STORI NA GABRIEL MUSHITecno


Toa comment