The House of Favourite Newspapers

Ne-Yo awaahidi Waganda shoo ya nguvu leo

0

STAA wa muziki wa R&B kutoka nchini Marekani, Shaffer Chimere Smith, Ne-Yo amewaahidi wananchi wa Uganda shoo ya nguvu leo usiku.

Ne-Yo aliyetua nchini Uganda jana, anatarajia kufanya shoo ya nguvu leo katika Tamasha la Bell Pop ‘N Jam litakalofanyika jijini Kampala.

Staa huyo ameyasema hayo wakati wa mkutano na wanahabari uliofanyika katika Hoteli ya Sheraton jijini Kampala leo asubuhi.

Ne-Yo aliwasili nchini humo jana saa 4:30 usiku kwa ndege ya Shirika la KLM na kuelekea katika Hoteli ya Sheraton alipolala na timu yake nzima ya watu 35.

Akihojiwa na wanahabari, Ne-Yo alikuwa na haya:

“Sikujua chochote nilipopata taarifa kuwa nina shoo nchini Uganda maana sikuwahi kufika katika
sehemu hii ya Afrika

“Mimi ni mtu wa wakati uliopo na ninapopata kazi ya kufanya; ninawaza kitu kilichopo na kuishi hivyo. Ninachoweza kuwaahidi ni kwamba nitaangusha shoo ya nguvu leo na ninawaomba mashabiki wangu mtarajie makubwa.”

Staa huyo bado anatamba na vibao vyake kama “So Sick,” “When You’re Mad” “Sexy Love” “Closer” na “Miss Independent”

Mbali na umahiri katika muziki, Ne-Yo pia ni mkali katika kutunga nyimbo aliyeibamba dunia pale alipomwandikia wimbo mwanamuziki wa Marekani, Mario uitwao “Let Me Love You” ulioshika namba moja katika Billboard Hot100.

Hii ni mara tatu kwa staa huyo kuja Afrika, Mwezi Julai alikuwa nchini Afrika Kusini wakati wa tuzo za MAMA, akatua nchini Kenya majuzi kwa ajili ya kipindi cha Coke Studio Afrika na sasa yupo ndani ya Uganda.

Leave A Reply