The House of Favourite Newspapers

NEC Yampitisha Lissu Kugombea Urais wa Tanzania – Video

0

MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Antipas Lissu ameteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwa mgombea wa Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho na mgombea mwenza wake Salum Mwalimu.

 

Akizungumza baada ya mapokezi ya fomu hizo, Mkurugenzi wa NEC, Dkt. Wilson Mahera, amesema  Magufuli na  Samia wametimiza vigezo vyote vya uteuzi na kuwania nafasi hiyo.

 

“Wagombea wamejaza kwa ukamilifu na kwa idadi inayotakiwa na ziada, wagombea wametoa tamko la kuwa wanazo sifa za kugombea, katibu mkuu wa chama ametoa tamko la uthibitisho wa kuwateua wagombea, wagombea wamedhaminiwa na wapiga kura katika mikoa 10 iliyokuwa ikiwemo ya Tanzania Bara na Zanzibar.

“Wasimamizi wa uchaguzi wamethibitisha majina ya wagombea, wagombea wametoa tamko mbele ya jaji kuwa wanazo sifa za kugombea, wamewasilisha stakabadhi ya dhamana ya Tsh milioni 1, wamewasilisha nakala picha nne za passport size kila mmoja, hapa tume tumekagua fomu zao za wadhamini na tumejiridhisha ziko sahihi, wametoa tamko la kutekeleza na kuheshimu maadili ya uchaguzi,” amesema Mahera.

 

“Baada ya kujiridhisha kwa mujibu wa sheria ya taifa ya uchaguzi na kwa mamlaka niliyopewa na Katiba ya nchi na kanuni za uchaguzi wa mwaka huu, tume ninatamka kuwa tume imewateua Dk. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu Hassan kuwa wagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema Kaijage.

 

Leave A Reply