NEC yakamilisha zoezi la kutangaza matokeo ya awali ya Urais

Jaji-Lubuva-620x309Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) leo imekamilisha zoezi la kutangaza matokeo ya awali ya Urais kwa majimbo yote 264 yaliyoshiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Akizungumza wakati wa kukamilisha zoezi hilo lililokuwa likifanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva amesema kuwa kazi ya kutangaza matokeo imekamilika, hatua inayofuata ni mawakala wa vyama, watazamaji na jeshi la polisi kwenda kujiridhisha na baada ya hapo kura zitajumlishwa.

Baada ya kura kujumlishwa tume itamtangaza mshindi katika uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Wakati tume ikikamilisha mchakato huo wa awali wa kutangaza matokeo, Mgombea Urais wa Chadema anayeungwa mkono na Ukawa, Edward Lowassa leo amewasilisha pingamizi lake kupinga matokeo hayo katika ofisi za Tume ya Uchaguzi.


Loading...

Toa comment