The House of Favourite Newspapers

Matokeo Ya darasa la nne na kidato cha pili, Yapo Hapa

Katibu mtendaji wa baraza hilo, Dk, Charles Msonde.

 

Baraza la Mitihani la Taifa (Necta)  Ijumaa Januari 4, 2019 limetangaza matokeo ya mtihani wa Taifa wa darasa la nne na kidato cha pili iliyofanyika Novemba 2018, kueleza kuwa ufaulu umeongezeka ikilinganishwa na matokeo ya 2017.

 

Akizungumza  mjini Dodoma katibu mtendaji wa baraza hilo, Dk, Charles Msonde amesema kati ya watahiniwa 1,302,461 wa darasa la nne waliofanya mtihani huo sawa na asilimia 95.58, waliofaulu kwa kupata daraja A, B, C, na D ni 1,213,132 sawa na asilimia 93.16.

 

Kutizama matokeo ya kidato cha pili >>>>> BONYEZA HAPA

Kutizama matokeo darasa la Nne >>>>> BONYEZA HAPA

 

Amesema wanafunzi 89,093 sawa na asilimia 6.84 wamepata alama za daraja E ambalo ni ufaulu usioridhisha.

“151 walishindwa kufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ugonjwa na utoro,” amesema.

 

Dk Msonde amesema mwaka 2018 takwimu za matokeo zinaonyesha kuwa ufaulu wa watahiniwa kwa masomo yote uko juu ya wastani.“Ubora wa ufaulu umezidi kuimarika kwa kuwa watahiniwa waliofaulu kwa daraja A, B na C umeongezeka kwa asilimia 0.03 ikilinganishwa na mwaka 2017,”amesema Dk Msonde.

 

Kuhusu kidato cha pili, Dk Msonde amesema watahiniwa 506,235 walisajiliwa kufanya mtihani huo sawa na asilimia 92.87, kwamba wanafunzi 38,842 sawa na asilimia 7.13 hawakufanya mtihani kutokana na ugonjwa na utoro.

 

Amesema wanafunzi 452,273 sawa na asilimia 89.68 wamepata alama za ufaulu zitakazowawezesha kuendelea na masomo ya kidato cha tatu.

 

Amesema wanafunzi 52,073 sawa na asilimia 10.32 wameshindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na masomo ya kidato cha tatu.

 

Amesema mwaka 2017 wanafunzi 433,453 sawa na asilimia 89.32 walipata alama za kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu, kwamba ikilinganishwa na 2018, ufaulu wa mwaka jana umeongezeka kwa asilimia 0.36.

Kutizama matokeo ya kidato cha pili >>>>> BONYEZA HAPA

Kutizama matokeo darasa la Nne >>>>> BONYEZA HAPA

Comments are closed.