The House of Favourite Newspapers

Necta Yazifungia Shule 24 kwa Kufanya Udanganyifu Mtihani la Saba …Ipo Rweikiza ya Bukoba, Al-hikma Dar

0
Kaimu Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani (NECTA), Athumani Amasi akitangaza matokeo ya mtihani wa elimu ya shule za msingi kwa mwaka 2022, jijini Dar es Salaam.

 

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) leo Desemba 1, 2022 limevifungia vituo vya mitihani 24 sawa na asilimia 0.13 ya vituo vyote 17,935 vilivyofanya mtihani ambavyo vimethibitika kupanga na kufanya udanganyifu katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi 2022.

Hayo yameleezwa leo Desemba Mosi na Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athuman Amasi wakati akitangaza matokeo ya mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka 2022.

 

Akizitaja shule hizo ni Kadama shule ya msingi iliyopo Chato- Geita, Rweikiza (Bukoba), Kilimanjaro shule ya msingi (Arusha) Sahare (Tanga), Ukerewe (Mwanza), Peaceland (Mwanza), Karume (Kagera), Al-hikma (Dar es Salaam).

 

Nyingine ni Kazoba (Kagera), Mugini (Mwanza), Busara (Mwanza), Jamia (kagera), Winners (Mwanza), Musabe (Mwanza), Elisabene (Songwe), High Challenge (Arusha), Tumaini (Mwanza), Olele (Mwanza), Mustlead (Pwani).

Pia zipo shule za Moregas (Mara), Leaders (Mara), Kivulini (Mwanza) na St Severine (Kagera).

“Vituo hivi vimefungiwa kwa mujibu wa kifungu 4(8) cha kanuni za mitihani mwaka 2016 hadi hapo Baraza litakapojiridhisha kuwa ni salama kwa uendeshaji wa mitihani ya kitaifa,” amesema.

Mtihani huo wa kumaliza elimu ya msingi ulihusisha watahiniwa zaidi ya 1.38 milioni nchi nzima.

BREAKING: AJALI MBAYA! LORI LAGONGA MAGARI 7 MWANZA, WATU KADHAA WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA….

Leave A Reply