NEEMA NABII ASIYEKUBALIKA

Neema Ndepanya

KWELI? Mwongozaji na mwigizaji wa Bongo Muvi, Neema Ndepanya amefunguka kuwa kwa kipindi kirefu alikuwa ni kama nabii asiyekubalika kwao kwani kila mtu hakumwelewa.

 

Neema ameliambia Gazeti la Ijumaa kuwa, alikuwa ana vitu vingi mno vya kuipeleka mbali tasnia ya filamu Bongo, lakini kila aliyekuwa akimfuata, alikuwa hamwelewi kabisa bila kujua walikuwa wanakosa madini yake.

 

“Hata Wema (Sepetu) mwenyewe mara ya kwanza hakunielewa, naona alijiuliza nimetokea wapi, lakini mwisho alijuta kwa nini alichelewa kuwa na mimi hasa kwenye eneo la ‘production’ ya sinema zake,” alisema Neema ambaye aliwahi kufanya kazi kwa karibu na staa mkubwa wa tasnia hiyo, Wema Isaac Sepetu

Toa comment