NELLY ANATAKA KUZAA LAKINI…

Nelly Kamwelu

WANAUME mpo? Mwanamitindo maarufu Bongo, Nelly Kamwelu amefunguka kuwa anataka sana kuwa na mtoto kwa kipindi hiki, lakini amejifunza kuwa mtoto bila malezi ya baba ni tatizo. 

 

Nelly aliliambia Gazeti la Ijumaa alipendalo kuwa, yeye ni mpenzi mkubwa wa watoto na kuna kipindi anatamani kubeba mtoto wake mwenyewe, lakini bila kuingia kwenye ndoa atavumilia tu.

 

“Natamani sana kuwa na mtoto, lakini nimejiwekea malengo kwamba bila ndoa, siwezi kuzaa nje ya ndoa, nahitaji kulea watoto wangu tukiwa wazazi wawili siyo kuwa peke yangu kwani hilo litaniumiza sana,” alisema Nelly ambaye aliwahi kuwa Miss Ilala na Mshiriki wa Miss Tanzania miaka ya nyuma.

Toa comment