Nelly kamwelu anunua lipstik kwa milioni 6

Na Musa Mateja

MREMBO aliyewahi kunyakua Taji la Dunia la Miss Universe, Nelly Kamwelu, juzikati alionesha jeuri ya pesa baada ya kutoa shilingi milioni 6 za Kitanzania kwa ajili ya kununua rangi ya mdomo (Lipstick) katika mnada uliofanyika wakati wa sherehe ya bethidei ya Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu.

Mrembo aliyewahi kunyakua Taji la Dunia la Miss Universe, Nelly Kamwelu.

Tukio hilo lilijiri usiku wa kuamkia Novemba 2, mwaka huu, ndani ya Ukumbi wa Wema Sepetu, uliopo ndani ya jengo jipya la Millennium Tower, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, ambapo Nelly aliwatikisa baadhi ya waalikwa kwa kufikia dau hilo wa mnada ulioendeshwa na meneja wa mrembo huyo, Martin Kadinda.

Baadhi ya mastaa wengine waliojaribu kupimana ubavu na msichana huyo, Linah, Vanessa Mdee, Esher Buheti na waalikwa wengineo, walijikuta wakitoa ahadi ya fedha kidogo, hivyo kumfanya kuwa mtu wa mwisho baada ya kutamka kutoa donge hilo.

Huo ulikuwa ni uzinduzi wa bidhaa mpya za muigizaji Wema, hafla iliyofanyika sambamba na sherehe ya bethidei yake, ambayo ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali walioalikwa, wakiwemo wanafamilia yake.


Loading...

Toa comment