The House of Favourite Newspapers

Nelly Muosha Magari wa Posta-10

0

Mpenzi msomaji, wiki iliyopita niliishia pale fundi Yassin alipokuwa akiagana na Zakayo na kumsisitiza sana kuwahi kufika kazini siku iliyofuata ambapo kijana huyo alimwambia angefanya hivyo. Je, kilifuatia nini? Songa mbele na chombezo hili tamu….

Kwa kuwa kituo cha mabasi ya Kisauke hakikuwa mbali walitumia kama dakika nne wakawa wamewasili ndipo fundi Yassin na Nelly walishuka wakaanza kuelekea Kituo cha daladala Kwa Ndevu kupanda gari la kwenda Mwenge ili wakaunganishe la Tandika.
Wakiwa wanatembea Nelly alikuwa akijiuliza mbona fundi Yassin hakumpatia fedha kama alivyofanya kwa wenzake!

Hata hivyo, kwa jinsi alivyokuwa akimfahamu fundi huyo alijua wakifika nyumbani angempatia ndipo akaanza kuifikiria safari yao tangu asubuhi alipokutana na yule mrembo kwenye DCM la kwenda Mwenge na wale wasichana waliopandia Kituo cha Jogoo walioshukia njia panda ya kwenda Kunduchi.

Kwa kuwa kichwani alikuwa na namba ya yule dada aliyekutana naye Mwenge, akazitamka kimoyomoyo, sifuri, saba, kumi na mbili, sabini na kumalizia ya mwisho akaachia tabasamu lililoonwa na fundi Yassin.

“Mwenzangu kimekufurahisha nini maana naona unatabasamu?” fundi Yassin alimwuliza Nelly.
“Bro bwana, kwani hujamuona yule dada alivyotuangalia kisha kuanza kutikisa makalio yake?” Nelly alimchomokea fundi Yassin.
“Hapana sijamuona, yupo wapi kwani?” fundi Yassin alimwuliza Nelly.
Kufuatia kuulizwa hivyo, Nelly alimwambia alikwishaondoka ndipo wakaendelea na safari hadi walipofika kituoni ambapo walipanda gari la kwenda Mwenge.

“Bro kweli kuna watu wapo vizuri sana duniani, wakati sisi tunafikiria hela ya kula wengine wanaporomosha majengo namna ile?” Nelly alimwambia fundi Yassin.
Baada ya Nelly kuuliza hivyo, fundi Yassin alimweleza kwamba maisha ndivyo yalivyo na watu wote hatuwezi kufanana, kauli ambayo iliungwa mkono na Nelly.

Akiwa ameketi siti ya dirishani, Nelly akaanza kumkumbuka Doreen hasa alivyokuwa akizichezea embe bolibo zake, si mkuu wake wa kaya akaanza kuchangamka.
Kijana huyo alipoangalia eneo la makazi ya mkuu wake wa kaya na kumuona alivyokuwa, akaachia tabasamu ambalo lilionwa na fundi Yassin ambaye alimwuliza alifurahishwa na nini!

Kwa haraka Nelly alimuonesha fundi Yassin mzee mmoja aliyekuwa amekaa siti ya kushoto kwao aliyekuwa amepitiwa na usingizi na kuacha kinywa wazi, Yassin alipomwangalia mzee huyo naye akaachia tabasamu bila kujua Nelly alimpiga changa la macho.

“Maisha dogo, unaweza kukuta tangu alipoondoka nyumbani kwake asubuhi hajanywa chai na huko alikokwenda hakijaeleweka hapo kajichokea mzee wa watu,” fundi Yassin alimwambia Nelly kwa kumnong’oneza.

“Ni kweli bro nakubaliana nawe,” Nelly alimwambia fundi wake.
Kama ilivyo kawaida ya mashorobaro kupenda mambo ya mademu na mambo mengine ya umri wake, wakati safari ikiendelea Nelly alikuwa akimtupia macho msichana mmoja denti aliyekuwa kabeba mkoba wake mkubwa mgongoni.

Denti huyo kwa alivyokuwa anamuona alimkadiria kuwa kidato cha tano au sita na alikuwa kaumbika vizuri licha ya kuwa ndani ya sare za shule, sketi aliyovaa ilionesha namna alivyojazia.

“Isingekuwa jela, mtoto mzuri kama huyu ni kulamba tu kwa kwenda mbele,” Nelly alijisemea moyoni baada ya kukitathmini kifua kitamu cha denti huyo kilichopambwa na viembe bolibo f’lani hivi.

Gari lilipofika kituo cha Interchick, waliingia watu kibao akiwemo msichana mmoja mweupe aliyekuwa kavaa suruali ya jeans na kitop cha njano, Nelly alipomtupia macho moyo wake ukapiga paa!

Wakati Nelly akiwa katika hali hiyo, fundi Yassin ambaye alikuwa akimfahamu vyema Nelly, alimbonyeza dogo huyo pajani, Nelly apomwangalia akamnong’oneza kwa kusema:
“Umeyaona mambo yako hayo?”
“Kaka nimeyaona, da mtoto kaumbika halafu mapigo kama haya ndiyo ugonjwa wangu mkubwa!” Nelly alimwambia fundi Yassin.

“Wewe si unajifanya mkali wa viumbe hawa, ukipata namba ya huyo dada au ukifanikiwa kuchonga naye nitakupa wekundu mmoja nje ya hela ya kazi,” fundi Yassin alimtania Nelly.

“Bro, masihara hayo!” Nelly alimwambia fundi wake.
“Siyo masihara, wewe fanya kama nilivyokuambia nikupe mpunga wako,” fundi Yassin alimwambia Nelly.

Kauli ya fundi Yassin ilimuweka katika wakati mgumu sana Nelly ambaye hakuelewa ataanzaje kuzungumza na yule msichana kisha kuipata namba yake ya simu!
“Sikubali nasema sikubali, kama mimi ndiye Nelly lazima nitaipata namba ya huyo mrembo kwanza hawa wapo duniani kwa ajili yetu,” Nelly aliwaza.

Baada ya kuwaza hivyo, Nelly alimuomba fundi Yassin ahamie upande wa dirishani, fundi Yassin huku akicheka akahamia siti ya dirishani.

Leave A Reply