The House of Favourite Newspapers

Nelly Muosha Magari wa Posta-18

0

Mpenzi msomaji, wiki iliyopita niliishia pale wazazi wa Nelly walipokuwa wakimzungumzia kijana wao huyo ambaye ilikuwa mara yake ya kwanza kwenda kufanya kazi za ujenzi na walipomuuliza kama angeendelea nayo akawaambia atafanya hivyo. Je, kilifuatia nini? Endelea na utamu huu…

Kule chumbani Nelly aliendelea kumuwaza Atu hasa alivyokuwa akiyazungusha macho yake mazuri na alivyokuwa akihema, akajikuta akisema peke yake kwamba watakapokutana Ijumaa waliyokubaliana atampa mambo matamu zaidi.

Hata hivyo, kutokana na ulevi aliokuwanao kichwani, hakuchukua muda mrefu alipitiwa na usingizi hata mama yake alipokwenda kumuamsha ili akale hakumsikia.

“Baba Nelly, kweli mwanao leo kachoka, nimemwita mpaka nikapata wasiwasi, nilipoingia kumwangalia yaani kalala fofofo,” mama huyo alimwambia mumewe.

“Ndivyo inavyotokea kwa mtu ambaye hajazoea kufanya kazi ngumu, muache akiamka atakula,” mzee Reli ya Uhuru alimwambia mkewe bila kujua kwamba Nelly licha ya kuchoshwa na kazi lakini zaidi ni kwa vile alitoka kumdungua kiumbe na pombe aliyokunywa.

Mpaka wazazi wake wanakwenda kulala, Nelly hakuamka hadi kulipokucha akawa wa kwanza kuamka na kujiandaa kwenda site na fundi Yassin, akiwa anaoga mama yake naye aliamka.

Alipomaliza kuoga na kutoka bafuni alimkuta mama yake akiwa anaweka mkaa jikoni kwa ajili ya kumwandalia chai baba yake, wakasalimiana ndipo mama mtu akamwuliza jana yake alikuwa kachoka sana?

“Yaani mama nilichoka balaa, lakini ndiyo kazi na maisha hayana njia ya mkato,” Nelly alimwambia mama yake.

“Nilijua tu ulichoka maana nilikuandalia chakula nikaja kukuamsha lakini hukunisikia kabisa, vipi nikupashie moto wali utakula alfajiri hii?”

Baada ya mama mtu kumwambia hivyo mwanaye, Nelly alimwambia asiwe na wasiwasi atakunywa site, mama hakuwa na la zaidi ndipo kijana huyo akaingia chumbani kwake kujiandaa.

Baada ya kujiandaa wakati anataka kutoka alikutana na baba yake wakasalimiana kisha alimuaga ndipo mzazi wake akamtakia kazi njema, Nelly akatoka na kuelekea kwa fundi Yassin.

Alipofika alimkuta fundi huyo akimsubiri na baada ya salamu wakaondoka bila kuwa na mzigo wowote kuelekea kupanda daladala la Mwenge, kwa bahati walikuta DCM tatu zikiwa zinasubiri abiria, wakapanda na kukaa siti ya pamoja.

Gari lilipojaa wakaanza safari ndipo fundi Yassin aliyekuwa na shauku ya kujua kilichojiri kati ya Atu na Nelly akaomba ampe mchapo huo, Nelly akaanza kumsimulia kwa sauti ya chini ili abiria wengine wasisikie.

“Wewe dogo sikuwezi, unatisha kuliko hata moto wa gesi,” fundi Yassin alimwambia Nelly baada ya kijana huyo kumpa mchapo wote na wakati huo walikuwa wamefika Magomeni.

“Kiasi tu bro, unajua wakati mwingine tunajenga heshima kwani huwezi kumuona mtoto mzuri kama yule halafu umuache tu, hivi unajua unaweza kulaumiwa hata huko mbinguni?” Nelly alimwambia fundi Yassin, wakacheka.

Hata hivyo, Fundi Yassin alimwambia Nelly aache utani wa kuhusisha mambo maovu na mbinguni, Nelly akagundua kosa lake na kutengua kauli yake, ambapo fundi Yassin akasema hapo sawa.

Kwa kuwa wakati walipokuwa wakipeana michapo walikuwa bize na jambo hilo, Nelly hakuwaona mabinti wawili wakali waliokuwa wamepandia Kigogo ambao walikosa siti hivyo kusimama pembeni yake.

Baadaye akawaona moyo ukamdunda pa kisha akambonyeza pajani fundi Yassin, fundi alipogeuka akamnong’oneza.“Wewe ndiyo unawaona muda huu, mbona wamepandia Kigogo?” fundi Yassin alimwambia Nelly kwa sauti ya kunong’ona pia.

“Sikuwaona mkuu, da watoto wakali sana hawa hasa huyu aliyevaa suruali ya jinzi, ana kifua kama ninavyovipenda.” Wakati wakiendelea na mazungumzo hayo, yule dada mwenye suruali ya jinzi alimuona na kubaini Nelly alikuwa kadatishwa na uzuri wake kwa makusudi mazima akajigeuza ili kumuonesha Nelly kiwowowo chake tata.

Baada ya msichana huyo aliyesimama pembeni ya kiti cha Nelly kujigeuza, Nelly akajikuta damu zikimwenda mbio kwani kihisia alimvua ‘viwalo’ dada huyo na kupata picha kama vile walikuwa chimbo, akapagawa kabisa.

Hata hivyo, Nelly alizidi kuumia kwani alishindwa hata kumsemesha mrembo huyo hadi walipoteremka kituo cha Vijana Kinondoni jambo lililomuweka Nelly katika wakati mgumu kwani alipanga kama wangefika mwisho wa safari lazima angeomba namba yake ya simu.
“Kaka leo umefeli, watoto wameshuka hata hai hujatoa!” fundi Yassin alimtania Nelly.
“We acha tu mkubwa wangu, ila tungefika mwisho ungeona ambavyo ningepewa namba yake kirahisi si unanijua lakini mi mdogo wako?” Nelly alimwambia fundi Yassin wakacheka.

Wawili hao waliendelea na stori hadi walipofika Mwenge wakapanda gari la Tegeta, wakiwa kwenye gari hilo Nelly akiwa anamuwaza Doreen ghafla fundi Yassin akamkatisha kwa kumuuliza alijisikiaje kufanya kazi za kifundi.

“Bro bwana! Kazi ni kazi tu na mtoto wa kiume hapaswi kuchagua kazi!” Nelly alimjibu fundi Yassin.

Leave A Reply