The House of Favourite Newspapers

Nelly Muosha Magari wa Posta-21

0

Mpenzi msomaji, wiki iliyopita niliishia pale Haruni aliyeshangazwa na tabia ya usharobaro wa Nelly alipomwambia Zakayo kwamba alihisi Nelly alikwishakuwa mwenyeji kuliko wao ndipo Zakayo akamwuliza alimaanisha nini?

Je, alipewa jibu gani?

Songa mbele na utamu huu…

“Hivi sisi tangu tulipoanza kazi hapa miezi miwili sasa na ushee tumewahi kuingia hata jikoni kwa bosi?” Haruni alimwuliza Zakayo.

Zakayo alimwambia hawakuwahi kisha alimfahamisha kwa jinsi alivyomuona, Nelly alikuwa ametoka ndani kwa bosi wao na ilivyoonesha hata chai alikuwa kanywa.
Alipowaeleza hivyo, fundi Yassin na Haruni waliishia kucheka kisha fundi akasema ndiyo mambo ya mjini yalivyo, ukiwa shapu mambo yatakunyokea na ukizubaa itakula kwako.

“Unamaanisha nini kaka mkubwa?” Zakayo akamwuliza fundi Yassin.
“Si nyie tangu mfike hapa mmejaa uoga sasa dogo kaja kishamzoea mtoto wa bosi na chai tena nzito kaanza kunywa,” fundi Yassin aliwaambia akina Zakayo walioishia kucheka.

Baada ya maongezi mafupi kuhusiana na Nelly, wakasikia mchanga ukilia tii wakajua dogo kishaanza kazi, kweli fundi Yassin alipokwenda kuangalia akamkuta Nelly akichota mchanga na kuusogeza sehemu aliyomwelekeza.

Kwa kuwa alitokea kwa nyuma, Nelly hakuweza kumuona akamwita, Nelly alipogeuka akacheka sana na kumwambia fundi wake kwamba pale ilikuwa kazi tu, fundi akaangua kicheko pia.

“Poa kaka, hapo kazi tu! Wewe endelea na kazi na sisi tunaendelea na kazi huku ndani,” fundi Yassin hakutaka kumweleza chochote alichoambiwa na Zakayo.

Fundi Yassin na vijana wake wakiwa wanaendelea na kazi, Zakayo aliyekuwa kama ameamka ghafla akamwambia fundi Yassin kwamba siku si nyingi Nelly angewaletea balaa pale site.

“Kwa nini unasema hivyo?” fundi Yassin alihoji.
“Kaka mkubwa huyu dogo hajatulia, siku bosi akirudi na kubaini anaingia ndani kwake na kunywa chai si atajua ana uhusiano na binti yake, wewe unafikiri tutapona kweli kama siyo kufukuzwa hapa?” Zakayo akamwambia.

Maneno ya kijana huyo yalimwingia vilivyo fundi Yassin aliyetegemea kupewa kazi kibao na bosi wake aliyekuwa kasafiri, lakini hakutaka kujibu chochote.

“Kwanza huyo dogo siyo mfanyakazi, tangu alipokuja hapa jana hakuna kazi aliyofanya, sasa ni hivi mkubwa, kama ataendelea kuja hapa site mimi naona ni bora niache kazi tu, yaani naiona hatari mbele yetu,” Zakayo alipiga mkwara.

“Poa Zakayo nimekuelewa sana, naomba kazi hiyo niachie mimi niliyemleta,” fundi Yassin alimwambia Zakayo.

“Lakini kaka mkubwa, nami naungana na mawazo ya Zakayo, mwenendo wa huyu dogo utatuponza, yeye kaja jana tu nyumba yote ya bosi kishaizoea na chai nzito ya kishua anakunywa!” Haruni naye akachombeza.

Kule chumbani, Doreen alikuwa kajilaza chali kitandani kwake kufuatia vionjo vya uhakika alivyopewa na Nelly, akapanga siku hiyo kumpa zawadi kama asante yake.
“Huyu kaka siyo siri anajua mapenzi, kama kwa muda mfupi tu niliokuwanaye kanipa raha namna hii, je tungekaa zaidi ya saa nne si ingekuwa balaa, huyu lazima nimpe zawadi,” Doreen aliyekuwa kavaa nguo ya mwisho pekee alijisemea moyoni.

Msichana huyo ambaye kwenye droo yake alikuwa na shilingi 200,000 alijiuliza ampatie laki moja au kwa kuwa Nelly hakuwa na simu ampatie simu yake ambayo alikuwa haitumii.

“Pesa hapana, kwa ninavyomuona anaweza asinunue simu ya maana ili zingine afanyie kazi nyingine, nampa simu,” Doreen aliwaza kisha aliinuka pale kitandani.

Kwa kuwa mbele yake palikuwa na kabati kubwa la kujipambia lililokuwa na kioo, wakati anajongea kwenye kabati hilo akacheka sana baada ya kuangalia kufuli alilokuwa amevaa na jinsi macho yalivyokuwa yamemlegea baada ya kulishwa tende na Nelly.

“Da! Huyu kaka kajua kunilegeza mtoto wa kike, zawadi inayomfaa ni simu tu ya kisasa,” Doreen akajisemea moyoni na kufungua droo ya kabati na kuchukua boksi la simu na kuliweka juu ya kitanda.

“Hii ndiyo zawadi pekee inayomfaa, kijana mzuri namna hii ataishije bila kuwa na simu, tena itarahisisha sana kuwasiliana naye kwani nitakapotaka kukutana naye hata nje ya hapa ni suala la kumpigia na kumwambia sehemu ya kumiti,” Doreen alijisemea moyoni.

Je, nini kilifuatia? Usikose Jumatatu ijayo. Maoni nicheki kupitia namba hizo hapo juu.

Leave A Reply