Nelly Muosha Magari wa Posta-26

Mpenzi msomaji, wiki iliyopita niliishia pale sharobaro Nelly alipotoka kuzungumza na rafiki yake Ipyana kuhusu kazi ya kuosha magari, aliporejea nyumbani na kumpatia shilingi elfu 15 mama yake na kumwambia za kununulia mboga. Je, kilifuatia nini? Songa mbele…

Wazazi wake walifurahi sana, baba alimsifia na kumwambia kweli alikuwa amekua na kumwuliza aliona faida ya kujishughulisha, akamwambia aliiona.

“Hivyo ndivyo kijana unatakiwa kuwa, wewe unafikiri nisingeshauri utafute kazi ya kufanya leo hii ungempatia mama yako hela ya kukununua mboga, safi sana tena sana,” baba yake Nelly mzee Reli ya Uhuru alimwambia.

Nelly aliwashukuru wazazi wake kisha aliwaaga kwamba alihisi uchovu hivyo anakwenda kulala, wakampa pole na kumtakia usiku mwema akaenda chumbani kwake bila kuwaambia kama fundi Yassin alimwambia asiende site.

“Hawa siwaambii chochote kuhusu ishu ya site, kukicha kesho naenda Posta ila nikitoka huko ndipo nitamwambia mama,” Nelly aliwaza.

Akiwa chumbani, alichukua simu aliyopewa na Doreen, akaweka kadi yake na kuiweka kwenye chaji huku akiwa mwenye furaha kwani hakutegemea kama angepata simu siku za karibuni.
“Tena ikipata chaji kidogo mtu wa kwaza kumpigia atakuwa Doreen, halafu nitampigia Atu na yule demu niliyekutana naye siku ya kwanza wakati tunaenda site,” Nelly aliwaza.

Kijana huyo akiwa kalala chali huku kavaa bukta pekee, alimlaani sana Zakayo kwa kumchongea kwa fundi Yassin na kusababisha kusimamishwa kufanya kazi kule site.“Ningekuwa mchawi ningemrogelea mbali Zakayo aanze kuumwa na kurudishwa kijijini kwao, au ningekuwa namiliki bastola ningempiga risasi za kichwa afie mbali kwa roho yake mbaya,” Nelly aliwaza.

Baada ya kutumia dakika kadhaa kumfikiria Zakayo, alipitiwa na usingizi hadi alipokuja kushtuka ilikuwa saa tano, alipoiangalia simu akakuta imejaa chaji fulu akaamua kumbipu Doreen.
Nelly alifurahi sana alipobaini Doreen alikuwa hewani, akiwa katika hali hiyo simu yake ikaanza kuita na mpigaji alikuwa Doreen akapokea.

“Sema mpenzi wangu, nimefurahi kweli ulivyonibip maana tangu nilipopanda kitandani mawazo yangu yote yalikuwa kwako, si unajua tena ulivyouteka moyo wangu kwa muda mfupi?” Doreen alimwambia.
“Hunishindi mimi, yaani kila nikikumbuka joto lako, mahaba yako na hizo embe zako zinazoshika vizuri, nimeshindwa kulala na simu ilipojaa chaji nikaamua kukupigia, yaani d sijui nikwambieje,” Nelly alimwambia Doreen.

Wawili hao walizungumza kwa muda mrefu kisha Doreen akamwuliza kama simu yake ilikuwa na vocha ya kutosha, Nelly akamwambia alinunua ya mia tano.

“Ngoja nikutumie muda wa maongezi wa kutosha ili tuchati hadi kuna kucha,” Doreen alimwambia.
Kama alivyomuahidi, baada ya kukata simu hazikupita hata sekunde 50 Nelly alisikia mlio wa ujumbe alipofungua akaona ametumiwa muda wa maongezi wa shilingi elfu tano.

“D, asante sana, haya niambie kitu kizuri sana nifurahi usiku huu,” Sharobaro Nelly akamwambia.
“Kitu kizuri ni kwamba nakupenda sana natakamani hata muda huu tungekuwa wote hapa kitandani ukinifanyia mambo yote mazuri ya kunipa raha,” Doreen alimjibu.

“Jamani mpenzi wangu, kwa kuwa uko mbali nami ndiyo hivyo, kama hutajali tukutane hapo kwa njia ya meseji,” Nelly akamwambia Doreen kupitia meseji.Doreen ambaye alikuwa akipenda sana kuchati alimwambia sawa ndipo sharobaro Nelly akaanza kumvurumishia meseji za kimahaba zilizomchanganya mtoto wa kishua na kujikuta yuko hoi.

Doreen alipomwambia Nelly kwamba alikuwa anajisikia ovyo, kijana huyo akaamua kumpigia wakaanza kuzungumza mambo ya malovee na kuhamasishana hadi Doreen akafikia kilele cha mlima wa Kilimanjaro kupitia simu zao.

Kufuatia Doreen kufika kilele cha mlima, alimfagilia sana Nelly kwa kujua kutumia simu yake maana ilikuwa kama walikuwa wote laivu, Nelly naye alimshukuru kwa ushirikiano wake, kisha waliagana kwamba wangekutana kesho yake.

Nelly alimwambia poa lakini hakutaka kumweleza kuhusu fundi Yassin kumzuia kwenda site, alipanga kumpigia simu mishale ya saa tatu ya siku iliyofuata kumweleza jambo hilo.

Kutokana na uchovu, msichana huyo akiwa kama alivyozaliwa akapitiwa na usingizi hadi aliposhtuka saa kumi na moja alfajiri, alipojiangalia na kukumbuka kilichojiri baina yake na Nell wakati wakichati akaishia kutabasamu.

Je, kilifuatia nini kwa wapenzi hao? Usikose mwendelezo wake wiki ijayo. Maoni, tumia namba hiyo juu.

Loading...

Toa comment