Nelly Muosha Magari wa Posta-7
Mpenzi msomaji, wiki iliyopita niliishia pale mtoto mkali Doreen alipombembeleza Nelly kwa sauti nyororo kwamba aliogopa nini kuingia ndani na kumsihi aingie kwani hakukuwa na tatizo. Je, baada kijana huyo sharobaro kuambiwa hivyo alisemaje? Tuwe pamoja kwenye utamu huu…
Kutokana na sauti nyororo ya kuhamasisha aliyoitoa Doreen, Nelly alijikuta akiwa jikoni mwa akina Doreen ambapo msichana huyo alimuongoza mpaka sebuleni kwao, kutokana na nguo aliyovaa kuchafuka kwa mchanga akawa hajui aketi wapi.
“Karibu ukae kwenye kiti,” Doreen alimwambia Nelly.
“Hapana sista wewe nipe nitakunywa wima, si unaona nilivyochafuka!” Nelly alimwambia Doreen.
Licha ya Nelly kutoa jibu hilo, Doreen ambaye ghafla alitokea kuvutiwa na kijana huyo kimapenzi kutokana na kupita muda mrefu bila kuduu alimlazimisha Nelly kukaa na kusisitiza kwamba hata kama sofa zingechafuka angemwambia Anne azifute.
Kitendo cha kubembelezwa kukaa na mtoto huyo ‘mtamu,’ Nelly alikaa sofani kitendo kilichomfurahisha sana Doreen ambaye alikwenda sehemu ya kulia chakula palipokuwa na jokofu na kuchukua jagi pamoja na glasi.
Alipomfikia Nelly alisogeza stuli iliyokuwa pembeni ya kochi na kuiweka glasi, akafungua jagi na kumimina juisi nzito ya embe, akachukua glasi na kumkabidhi Nelly aliyebakia kaduwaa.
“Wewe si ulitaka maji, mimi nimependa unywe hii juisi,” Doreen mtoto aliyeumbwa haswa na kujaliwa kuwa na makalio f’lani hivi ya kiuchokozi alimwambia Nelly.
“Da! Sikutegemea kama leo nitakutana na sapraizi ya namna hii, sina cha kuongezea zaidi ya kushukuru kwa ukarimu huu ambao sijapata kuuona,” Nelly alimwambia Doreen.
Wakati Nelly na Doreen wakipiga stori ndani, si fundi Yassin, Zakayo wala Haruni aliyekumbuka habari za Nelly kwani wakati huo walikuwa bize kwa kazi ya kuweka malumalu.
“Kuwa huru tu kaka, hapa nyumbani tumebaki wawili tu mimi na dada,” Doreen alimwambia Nelly huku akiwa anakwenda sehemu ya kulia chakula palipokuwa na kabati kubwa la vioo lililokuwa na vyombo.
Kwa kuwa muda huo, msichana huyo alivaa pensi iliyombana vyema na kusababisha wowowo lake la kiuchokozi kuonekana na blauzi nyepesi mfano wa singilendi kuonesha viembe sindano vyake, Nelly akachanganyikiwa kabisa.
“Aaa…duuu…aaa…,” Nelly alijikuta akiguna akiwa amelitumbulia macho eneo la nyuma la Doreen na kushindwa kuendelea kunywa juisi.
Doreen ambaye hakuwa na habari na kilichokuwa kikijiri nyuma yake, alipolifikia kabati la vyombo alisukuma vioo vya ‘kusilaidi’ na kutoa glasi lakini ile anageuka Nelly alijifanya anakunywa juisi.
“Ngoja na mimi nikusaidie,” Doreen alimwambia Nelly wakati akimimina juisi kwenye glasi yake kisha akaketi kwenye sofa aliloketi Nelly.
Kitendo cha msichana huyo kuketi karibu na sharobaro Nelly, kijana huyo alizidi kuchanganyikiwa ndipo Doreen alimwuliza kama kweli alikuwa fundi au alikuja pale kumpeleleza baba yake.
“Hapana sista, mimi nije kumpeleleza baba yako ili iweje wakati simfahamu na ndiyo mara yangu ya kwanza kufika hapa?” Nelly alimwambia Doreen.
“Ulivyo na kazi unayoifanya vitu viwili tofauti, lazima nikutilie shaka,” Doreen alimwambia Nelly.
“Naomba usinifikirie hivyo, mimi siyo mpelelezi,” Nelly alimwambia Doreen.
Baada ya Nelly kumhakikishia hivyo Doreen, msichana huyo alitabasamu na kumwambia kama ni kweli itakuwa vizuri ndipo alimwuliza sababu za kuchagua kazi ya ufundi.
“Maisha tu dada, ila nilitamani sana kukaa ofisini niwe nafanya kazi kwa kutumia kompyuta lakini ndiyo hivyo,” Nelly alimwambia Doreen.
Kufuatia kijana huyo kumwambia hivyo, msichana huyo alimwuliza alifika kidato cha ngapi, Nelly alimwambia cha nne na kumweleza kila kitu hadi kufikia hatua ya kuwa pale.
“Unataka kuniambia leo ndiyo mara yako ya kwanza kufanya kazi ya ufundi?” Doreen aliyemuonea huruma Nelly alimwuliza.
“Ndiyo hivyo,” Nelly alimjibu.
Baada ya kijana huyo kujibu hivyo, Doreen alikubaliana naye kwani alimuona jinsi alivyokuwa akijinyoosha kila alipochota mchanga na kuutupia eneo aliloelekezwa na Zakayo.
“Oke, sasa sina shaka na wewe, naomba nikuongeze juisi,” Doreen aliyepania kufikia hatua f’lani na Nelly alimwambia.“Nashukuru sista inatosha,” Nelly alimwambia Doreen.
Licha ya kukataa, Doreen alimimina juisi na kujaza glasi aliyokuwa akitumia Nelly, lengo lake lilikuwa kumchelewesha kwani aliamini kitendo cha kuwa pamoja na Nelly angemtongoza tu!
“Ila wewe dada ni mkarimu sana, nashukuru kwa kunijali,” Nelly alimwambia Doreen huku moyoni akipanga kumtongoza kwani hakuwa na sera ya kumuacha msichana mrembo kama Doreen.