The House of Favourite Newspapers

Nelly Muosha Magari wa Posta-8

0

 Mpenzi msomaji, wiki iliyopita niliishia pale Nelly alijiandaa kumchinjia baharini mtoto mzuri Doreen ambaye alikuwa amelainika kupita maelezo na muda huo kuhitaji kitu kimoja tu ‘mkomboti’, lakini akasikika akiitwa na Zakayo. Je kilifuatia nini? Songa nayo…

Kufuatia sharobaro Nelly kuitwa, aliipandisha fasta suruali yake juu ambayo alikuwa ameiteremsha hadi magotini, Doreen naye alisimama pale sofani na kuchukua nguo zake na kukimbilia chumbani.

Zakayo aliendelea kuita ndipo Nelly alitoka haraka pale sebuleni na kwenda jikoni kwa akina Doreen, Zakayo alipoona kijana huyo haitiki alijua alitoka nje ya geti akarudi kumfahamisha fundi Yassin kwamba hakuwepo.

Nelly alipoona Zakayo kaondoka alivuta pumzi na kuzishusha akafurahi kwani alijua atakapokuwa akitoka mle ndani asingeonekana, wakati akiwaza hivyo Doreen ambaye tayari alivaa nguo alikwenda na kumshika Nelly begani.

“Vipi, amejua kama upo humu ndani?” Doree ambaye macho bado yalikuwa yamemlegea alimwuliza.

“Hajaniona na kaingia ndani,” Nelly ambaye alimlaani sana Zakayo kumkatishia starehe yake alimwambia  Doreen.

“Kama hajakuona vizuri, ili kuwapoteza maboya itabidi nikutoe nje kabisa kwa kutumia mlango huu wa uani, baadaye ugonge geti ujifanye ulikwenda kununua soda,” Doreen alimwambia Nelly.

“Sasa hiyo soda nitanunua na hela gani wakati kwenye suruali yangu iliyopo ndani kuna shilingi mia tano tu!” Nelly alimwambia mrembo huyo.

Baada ya kutoa kauli hiyo, Doreen alicheka akamwambia asubiri akaingia ndani kisha kutoka akiwa na soda ya kopo akamwambia atoke nayo nje ili atakapofunguliwa geti ionekane alitoka kuinunua.

“Du! Kweli wewe mjanja sana,” Nelly alimwambia Doreen kisha aliichukua ile soda ya kopo lakini kabla ya kutoka nje akaona hatakuwa amemtendea haki msichana huyo bila kumbusu.

“Jamani asante yaani busu lako limenisisimua sana,” Doreen alimwambia Nelly akiwa kamkumbatia bila kujali nguo zake zilizochafuka kwa michanga.

“Ila basi tu, huyu aliyeniita katuvurugia sana nilitaka kukuonjesha penzi langu,” Nelly alimwambia Doreen.

Wawili hao wakiwa wanazungumza, Zakayo akiwa nyuma ya nyumba waliyokuwa wakiweka marumaru akaanza kumwita tena Nelly, bila kuchelewa Doreen alifungua mlango mdogo wa uani na kumtoa Nelly.

Baada ya Nelly kutoka, Zakayo akaendelea kumwita ndipo kijana huyo aliitika akiwa nje ya nyumba, Zakayo alipomsikia akiitika alikwenda kufungua geti akamkuta Nelly ameshika soda ya kopo.

“Kaka muda sasa tunakutafuta kumbe mwenzetu umeacha kazi na kwenda kununua soda, hivi utaiweza kazi hii tunayofanya?” Zakayo alimwuliza Nelly.

“Unajua muda ule sista sijui Doreen kanipa maji nikaendelea na kazi nikaona kiu bado imenishika nikaamua kwenda kununua hii soda kwani huwa nikinywa kidogo inakata kiu,” Nelly alimwambia Zakayo.

Zakayo alimtazama Nelly  alivyokuwa akizungumza na ile soda yake ya kopo aliyokuwa ameishika akaishia kucheka na kujisemea moyoni;

“Kweli site imevamiwa na sharobaro, sisi tunawaza kazi yeye tayari kisha kuwa mwenyeji mpaka kaenda kununua soda ya kopo, kweli huyu dogo ni mtoto wa mama.”

Kwa kuwa walikuwa wakizungumza wakiwa wamesimama pale getini, Zakayo alilifunga kisha wakaongozana kuingia ndani na kwenda moja kwa moja katika chumba ambacho fundi Yassin na wasaidizi wake hao walikuwa wakifanya kazi.

Fundi Yassin alipomuona Nelly kashika soda ya kopo, awali alifikiria alipewa na Doreen lakini Zakayo akamweleza jinsi Nelly alivyokuwa mwenyeji mpaka kutoka nje na kwenda kununua soda.

“Yaani alikuwa nje kabisa ya geti?” fundi Yassin alimwuliza Zakayo huku Haruni akiwa amepozi kufanya kazi akimsikiliza.

“Ndiyo maana yake, si nilikuja kuwaambia nimemwita lakini hakuitika, niliporudia kumwita kwa mara ya pili, nikamsikia akiitika nje ya geti,” Zakayo aliwaambia.

Fundi Yassin alimkanya Nelly kwamba kilichompeleka pale ni kazi na kumfahamisha jinsi tajiri yao asivyopenda watoke getini ndiyo maana aliwaambia chochote watakachohitaji wamwambie Anne ambaye ni dada wa kazi.

“Basi bro potezea sikujua, kwa hiyo nikisikia njaa nimwambie  huyo dada,” Nelly aliwaambia na kusababisha wote kuangua kicheko.

Wakati mafundi hao wakizungumza hivyo, Doreen akiwa chumbani kwake mawazo yote yalikuwa kwa Nelly kwani kijana huyo alijua kumsisimua sana.

“Huyu mkaka anavyoonekana mambo anayaweza, yaani hapa kaniacha mwili wote una ninyevuanyevua, asingeitwa na yule fundi saizi angekuwa kisha nipa raha, na nilivyomisi nanii da!” Doreen aliwaza.

Baada ya Nelly kuwachekesha mafundi wake alitoka akiwa kashika soda yake ya kopo na kwenda kuendelea na kazi, ambapo aliiweka ile soda juu ya dirisha bila kujua kama Doreen alikuwa kasimama katika dirisha hilo kwa ndani akimwangalia.

Leave A Reply