The House of Favourite Newspapers

NEMC Yatembelea Safu za Milima Ya Nyanda za Juu Kusini

0
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limefanya ziara katika safu za milima ya livingstoni iliyopo Nyanda za juu Kusini kwa lengo la kujiridhisha na changamoto za kimazingira zinazosababishwa na shughuli za kibinadamu ili kutafuta namna bora ya kukabiliana nazo ili kuyalinda kwa mstakabali mzima wa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt Samweli Gwamaka amesema lengo pia ni kutekeleza agizo la Mhe.Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania la kuvitaka vyanzo vya maji kulindwa ili kuepukana na athari za kimazingira kubwa likiwa uharibifu wa uoto wa asili.
Amesema uharibifu mkubwa wa mazingira unaosababishwa na shughuli za kibinadamu ni janga kubwa linalotakiwa kudhibitiwa ili kuepuka ongezeko la uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji hali itakayopelekea athari kubwa za kimazingira katika safu za milima hii ya nyanda za juu Kusini.
Amesema” wananchi wamekuwa wakivunja Sheria kutokana na shughuli za kibinadamu, hivyo niombe mamlaka za misitu, wadau wa mazingira, Halmashauri za vijiji na Miji tuzidishe utoaji  elimu katika sekta hii ili kunusuru vyanzo vyetu vya maji”. Dkt Samuel Gwamaka.
Amesema NEMC kama mdau mkubwa wa mazingira mwenye jukumu la kusimamia Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake ni wajibu wake kuhakikisha vyanzo vya maji vinalindwa ili kuepukana na athari za uharibifu wake kama  mafuriko, kuharibiwa kwa ikolojia za ardhi, wanyama na mimea, kuharibu uoto wa asili pamoja na kusababisha kukosekana kwa maji.
Katika ziara hiyo iliyojumuisha wataalamu wa Mazingira kutoka NEMC, TFS  na Afisa Maliasili wa Halmashauri husika, imetembelea Mkoa wa Mbeya wilaya ya Rungwe, Halmashauri ya Busokelo na Halmashauri ya Kyela.
Leave A Reply