Nenda Dar Live Ushuhudie Kombe la Dunia 2018

WAPENZI wa soka hapa nchini, watapata nafasi ya kushuhudia ‘live’ michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Urusi kupitia luninga kubwa wakiwa sehemu tulivu katika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam.

 

Hayo yamesemwa na Meneja wa Dar Live, Rajab Mteta ‘KP’ alipozungumza na Championi Jumatano ambapo michuano hiyo inatarajiwa kuanza kesho Alhamisi na kumalizika Julai 15, mwaka huu.

“Tutaonyesha mechi zote za Kombe la Dunia, hivyo mashabiki waje kwa wingi Dar Live sehemu ambayo ni tulivu waweze kushuhudia mechi hizo.

 

“Wakiwa hapo watapata huduma zote za vinywaji na chakula bila ya kusahau muziki, hivyo tunawakaribi­sha wote,” alisema KP.

 Mwandishi Wetu | Dar es Salaam

Shughuli itakuwepo Dar Live kuanzia keshokutwa Alhamisi June 14.

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on


Loading...

Toa comment